Afrika

China kusaidia mataifa yanayoendelea katika kilimo

Shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO, limesema kwamba China imeingia katika jumuia ya wafadhili wa kuu wa shirika hilo, kwa kutoa dola milioni 30 kuanzisha fuko maalumu la kuimarisha uzalishaji chakula katika nchi zinazoendelea.

UNHCR imegundua ni Wangola wachache wanaotaka kurudi nyumbani

Utafiti mpya wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la UM UNHCR, na serekali ya Zambia umegundua kwamba ni wakimbizi 251 wa ki-Angola kati ya elfu 10 katika kambi ya wakimbizi ya Mayukwayukwa, wenye haja ya kurudi nyumbani mwaka huu licha ya kampeni inayowahimiza kufikiria kurudi nyumbani.

Mahojiano na Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya Hassan Omar

Muasisi wa kundi la kutetea Haki za Binadamu "Oscar Foundation", Oscar Kamau Kingara aliuliwa pamoja na mshauri wake wa habari John Paul Oulu wakiwa garini karibu na chuo kikuu cha Nairobi.

UNICEF kuwachanja watoto Rwanda

Wizara ya afya ya Rwanda ikisaidiwa na shirika la Watoto la UM, UNICEF, imezindua kampeni ya pili ya wiki moja, kuwahi kufanywa nchini humo ya kuwapatia kinga watoto na kina mama kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuiliwa kwa urahisi.

Watu saba wapoteza maisha katika ajali nje pwani ya Yemen.

Kiasi ya wahamiaji saba wa Kiafrika walizama na kufariki mwishoni mwa wiki wakati meli ya biashara ya magendo walokua wanasafiria ilipozama muda mfupi tu baada ya kutia n\'ganga kwenye bandari ya Aden huko Yemen.

Mjumbe maalum apongeza mkataba na waasi huko DRC

Mjumbe maalum wa UM huko JKK amesifu makubaliano yaliyotiwa sahihi Ijumatatu kati ya serekali ya Kinshasa na kundi la waasi lililokua likiendesha mapigano yaliyosababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao huko mashariki ya nchi mwaka jana.

Ban anasema kiwango cha uwambukizaji wa kifua kikuu kinapungulia

Akiadhimisha siku ya kifua kikuu duniani hii leo, KM Ban Ki-moon amesema kasi za kupungua ugonjwa wa kifua kikuu zinakwenda pole pole na kuonya kua juhudi za kupambana na ugonjwa huo zinapunguka.

Rais wa Sudan atembelea Eritrea bila ya kukamatwa

Rais Omar Al-Bashir wa Sudan amabae amefunguliwa mashtaka na Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa, ICC, alipokelewa na kiongozi mwenzake Isaias Afwerki wa Eritrea na wananchi, licha ya kwamba kuna hati ya kimataifa ya kukamatwa kwake.

Pendekezo la FAO la Mkutano wa Viongozi juu ya Mzozo wa Chakula lapata Nguvu

Shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO, limesema kwamba pendekezo la kuitisha mkutano wa viongozi duniani mwishoni mwaka 2009 juu ya mzozo wa chakula, ambao unazidi kuzorota katika nchi maskini, linapata nguvu na kupewa umuhimu mkubwa.

UM yaadhimisha Siku ya Utabiri wa Hali ya Hewa

Ikiadhimisha siku ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani leo Jumatatu, Idara ya UM ya kutabiri hali ya hewa WMO, inazingatia juu ya uchafuzi wa hewa duniani, kutokana na takwimu kwamba, kiasi ya watu milioni mbili duniani hufariki mapema kutokana na hewa chafu kila mwaka.