Leo asubuhi, kwenye Ukumbi wa Mikutano, wa rakamu ya tatu, kulisanyika wajumbe wa kimataifa kwenye kikao maalumu cha wawakilishi wote, kusikiliza fafanuzi za KM Ban Ki-moon, na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dktr Margaret Chan juu ya maandalizi ya kimataifa ya kudhibiti bora mripuko wa virusi vya homa ya mafua ya aina ya A(H1N1).