Afrika

KM ahimiza uhusiano imara kati ya UM na AU

Jopo la pamoja la UM na AU kutayarisha mkakati wa ushirikiano kati ya jumuia hizo mbili hasa katika masauala ya kulinda amani limewasilisha ripoti yake mbele ya Baraza la uUalama.

UM unatafuta dola milioni 244 kuimarisha msaada wa chakula Kenya

Idara ya Chakula Duniani WFP, imetoa mwito Jumatano wa kuchangisha dola milioni 244 ilikuimarisha kazi zake huko Kenya, ambako bei za juu za chakula na ukame zimesababisha watu milioni 3 na nusu kuhitaji mdsaada.

Mpango wa dola milioni 18 UM kusaidia mataifa matano kupunguza gesi za sumu

Mataifa matano ya Afrika, Asia na Amerika ya Kati yatapokea jumla ya dola milioni 18 kutoka mradi mmoja wa majaribiyo wa UM wenye lengo la kupunguza gesi za sumu za greenhouse kutoka misitu na kuimarisha hali ya maisha ya wakazi.

Matumaini ya mafanikio kwenye mkutano wa ubaguzi mwezi ujao

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa UM, BI Navi Pillay, ameeleza matumaini yake Ijumatano ya kuwepo na maridhiano miongoni mwa mataifa wanachama kwenye mkutano wa mwezi ujao wa kupambana na ubaguzi, kutokana na kutolewa mswada mpya mfupi wa rasimu ya hati ya mwisho ya mkutano.

UNAIDS yahimiza mipango ya mchanganyiko kupambana na UKIMWI

Kukiwepo na zaidi ya watu 7 400 kila siku wanao ambukizwa na virusi vya HIV, shirika la kupambana na UKIMWI la UM UNAIDS, linasema ni lazima kuwepo na mkakati wa kIchanganyiko ikiwa ni pamoja na utumiaji mipra ya kondom kama chombo muhimu kuzuia kuenea kwa janga la UKIMWI.

Msaada wa Japan kwa kusaidia kukabiliana na athari za mzozo wachakula Africa

Msaada wa dola milioni 16 kutoka kwa serekali ya Japan, utaweza kulisaidia shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, kukabiliana na baadhi ya athari kutokana na mzozo mkubwa wa chakula unaowakabili wahamiaji huko Pembe ya Afrika pamoja na Mashariki na Kusini ya bara hilo.

Mlinda Amani wa UNAMID auliwa huko Darfur

Mlinda amani wa kikosi cha pamoja cha UM na Umoja wa Afrika UNAMID huko Drafur ameuliwa katika shambulio la kushitukiza.

Kamishna wa Haki za Binadamu anatoa ripoti juu ya kazi zake DRC

Naibu kamishna wa Haki za Binadam alitoa ripoti ya kamishna mkuu juu ya hali ya haki za binadam na kazi za afisi hiyo huko JKK.

Rais wa Madagascar astahafu na kukabidhi majeshi madaraka

KM Ban Ki-moon amezihimiza pande zote huko Madagascar kuhakikisha utulivu na mpito makini wa kidemokrasiakufuatia kujiuzulu kwa rais Marc Ravalomanana.

UM unajaribu kuachiliwa huru watumishi wake waliotekwa Somalia

Afisi ya UM ya kuratibu huduma za dharura huko Somalia inasema inatafuta njia za kuachiliwa huru bila ya masharti yeyote wafanyakazi wanne wa afisi hiyo walotekwa nyara Jumatatu asubuhi na washambulkizi wasojulikana.