Afrika

WFP imeanza operesheni za kuhudumia chakula wakazi waliotengwa na mvua kali Kaskazini-Mashariki katika JKK

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeanza kudondosha vyakula, kutoka kwenye ndege, katika eneo la Dungu, kaskazini-mashariki katika JKK kwa lengo la kuwaokoa njaa wahamiaji 130,000 waliong\'olewa makazi pamoja na wenyeji wao, ambao wameng\'olewa makazi na kutenganishwa baada ya mvua kali kunyesha karibuni kwenye maeneo yao.

UM inasema raia katika JKK wanaendelea kuteswa kihorera

Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Dharura (OCHA) imetoa taarifa yenye kusema kuna ushahidi baadhi ya wanajeshi wa vikosi vya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (FARDC) hushiriki kwenye vitendo vya kunyanganya kwa nguvu na kunajisi kimabavu raia, na wakati huo huo kuendeleza mauaji ya raia, halkadhalika, katika eneo la kaskazini-mashariki ya nchi.

Operesheni za kuwarejesha wahamiaji wa Burundi zaihusisha UNHCR

Mapema wiki hii, Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) Ijumatatu lilishiriki kwenye juhudi za kuwarejesha Burundi wahamiaji 529, kutoka kambi ya Kigeme, iliopo kwenye Wilaya ya Nyammgabe katika Rwanda kusini.

Wahusika wingi wanatakikana kutekeleza sera za kupunguza silaha duniani, anasema KM

Wajumbe wa kimataifa wanaohudhuria Mkutano wa Upunguzaji Silaha Geneva, walinasihiwa na KM Ban Ki-moon kwamba kunahitajika kuwepo mwelekeo unaohusisha pande mbalimbali pindi wamewania kuwasilisha kidhati maendeleo yanayosarifika kwenye zile juhudi za kupunguza silaha duniani.

Mkuu wa WHO anasema taarifa inayoaminika ya H1N1 ni muhimu kutuliza wahka wa umma kimataifa

Dktr Margaret Chan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la WHO, kwenye mashauriano ya kiwango cha juu kuhusu maambukizi ya homa ya mafua ya A(H1N1) yaliofanyika Geneva Ijumatatu, alitilia mkazo umuhimu wa kuripoti "taarifa halisi za kitaaluma, zinazoaminika, juu ya vipengele mbalimbali vilivyodhihiri kuhusu ugonjwa huu, na kuwawezesha wataalamu kufanya maamuzi ya dharura ya kudhibiti bora mfumko wa maradhi kwa kujitayarisha kukabiliana na janga hilo kimataifa."

Makampuni ya madawa yaombwa na KM kushirikiana kimataifa kudhibiti vyema homa ya A(H1N1)

KM Ban Ki-moon kwenye risala yake mbele ya kikao cha 62 cha Baraza Kuu la Afya Duniani, kilichofunguliwa rasmi mapema wiki hii mjini Geneva, aliyahimiza makampuni yenye kutengeneza madawa kushirikiana na serikali wanachama katika kutafuta suluhu ya dharura, ili kuulinda ulimwengu na maambukizi hatari ya mripuko wa karibuni wa maradhi ya homa ya mafua ya A(H1N1).

Kikao cha mwaka cha wenyeji wa asili kimefunguliwa rasmi Makao Makuu

Tume ya Kudumu ya UM juu ya Masauala ya Wenyeji wa Asili (UNPFII) imeanzisha kikao cha mwaka, kitakachokua karibu wiki mbili, kwenye Makao Makuu ya UM na kuendelea mpaka tarehe 29 Mei (2009), kwa makusudio ya kusailia taratibu za kuharakisha utekelezaji wa Mwito wa Kimataifa juu ya Haki za Wenyeji wa Asili.

BU, Umoja wa Afrika waafikiana kuimarisha ushirikiano

Mwisho wa wiki iliopita, mnamo Ijumamosi ya tarehe 16 Mei (2009), wajumbe wa Baraza la Usalama wa kutoka Makao Makuu ya UM, walipokuwepo Addis Ababa, Ethiopia kwenye ziara yao ya Afrika, walikuwa na mazungumzo na wawakilishi wa Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Afrika ambapo waliafikiana kushauriana, kwa ukaribu zaidi, na kushirikiana kwenye juhudi za kuzuia na kusuluhisha mizozo iliyotawanyika Afrika kwa sasa, na vile vile walikubaliana kujumuisha mchango wao katika huduma za kulinda amani na kudumisha utulivu kwenye maeneo yote husika.

Takwimu za WHO juu ya Homa ya A(H1N1)

Takwimu mpya za Shirika la Afya Duniani (WHO) juu ya maambukizi ya homa ya mafua ya A(H1N1) zinasema nchi 34 zimethibitisha rasmi kugundua wagonjwa waliopatwa na maradhi haya kwenye maeno yao.

Hali ya mapigano Mogadishu inachukiza na lazima ikomeshwe haraka, inasema UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeeleza kutoridhika na kuselelea kwa hali ya mapigano, vurugu na fujo katika Usomali kwa sasa.