Afrika

Mkariri anayehusika na mauaji nje ya taratibu za kimahakama atazuru Kenya

Philip Alston, Mkariri wa UM juu ya masuala ya mauaji ya kihorera, nje ya taratibu za kimahakama, anatazamiwa kuzuru Kenya kuanzia tareh 16 mpaka 25 Februari, kwa kuitika mwaliko wa Serikali ya Kenya na atakapokuwepo huko atakutana na maofisa wa Serikali kuu na pia zile za majimbo, na vile vile atakutana kwa mashauriano na wabunge.

Wahamiaji 25,000 wa JKK katika Zambia waiomba UM iwarejeshe makwao

Shirika la UM Juu ya Wahamiaji (UNHCR) limeripoti asilimia 99 ya wazalendo wahamiaji 25,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK), waliopo kwenye kambi za Kala na Mwanga, nchini Zambia wameomba warejeshwe makwao na UM. Kambi hizi mbili zipo katika eneo la Zambia kaskazini, kilomita 1,000 kutoka mji mkuu wa Lusaka.

Mahakama ya ICC inakana tetesi za kufikia uamuzi wa kumshika Raisi wa Sudan

Mahakama ya Kimataifa juu ya Jinai ya Halaiki (ICC) imetangaza taarifa maalumu, inayokana zile tetesi zilizosambaa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, zinazodai kwamba mahakimu wake wamefikia uamuzi wa kutoa hati ya kumshika Raisi Omar Al Bashir wa Sudan.

Kamishna wa Haki za Binadamu aisihi Zimbabwe kufufua utaratibu wa kuhishimu sheria

Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu, Navi Pillay, ametoa mwito maalumu uliopendekeza kwa Serikali mpya ya Muungano wa Taifa katika Zimbabwe, kuchukua hatua za dharura kufufua taratibu za kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa na kuhishimiwa na kila raia.

Uzalishaji wa nafaka unaashiriwa na FAO kuporomoka kwa mwaka huu

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) limewakilisha ripoti inayozingatia hali ya uzalishaji wa nafaka, kwa mwaka huu, katika dunia.

UNODC imewakilisha ripoti mpya kuhusu biashara ya magendo ya kuchuuza watu wanaotoroshwa

Shirika la UM juu ya Udhibiti wa Madawa ya Kulevya na Uhalifu (UNODC) limewasilisha "Ripoti ya Dunia juu ya Utoroshaji Magendo wa Watu kwa 2007 - 2008".

Baraza la Usalama linazingatia Chad na JAK

Baraza la Usalama Ijumaa limezingatia ripoti ya karibuni ya KM juu ya hali ya usalama katika Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati (JAK). Ndani ya ripoti KM amependekeza UM upeleke vikosi vya kulinda amani vya UM vya wanajeshi 6,000 wanaotakikana kuchukua nafasi ya vikosi vya Umoja wa Ulaya viliopo Chad mashariki na kaskazini-mashariki ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, maeneo ambayo katika miaka ya karibuni yaliharibiwa na fujo na vuruguu, na kusababisha halaiki ya raia kungo’lewa makazi na kuelekea kwenye maeneo mengine walipopatiwa uhamisho wa muda.~