Afrika

Ban anapongeza kuachiliwa mfanyakazi moja wa UM huko Niger

KM Ban Ki-moon amepongeza hii leo kauchiliwa huru mfanaykazi mmoja wa UM aliyetekwa nyara Niger mwishoni mwa mwaka jana na akarudia tena mwito wake wa kuachiliwa huru wafanyakazi wengine wawili pamoja na mwakilishi wa UM nchini humo, Robert Fowler kutoka Canada.

KM anasema ni lazima dunia kufanya kazi pamoja kutumia maji kwa busara

KM wa UM Ban Ki-moon amesisitisza umuhimu wa maji kama nguvu za kungana pamoja kuliko kiungo cha mizozo, akihimiza kwamba mustakbala wa pamoja wa dunia unategemea jinsi inavyosimamia rasilmali yake hii tunu.

Mahojiano na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, na Watoto, ya Tanzania Bi. Mariam Joy Mwaffisi

Wajumbe kwenye mkutano wa Kamisheni juu ya Hali ya Wanawake walijadili kwa mapana marefu namna ya kuhamasisha haja ya wanawake na wanaume kufanya kazi pamoja katika majukumu ya malezi, kuwahudumia waathiriwa wa HIV na Ukimwi, pamoja na majukumu ya nyumbani.

Mvua kali ya tishia mafuriko zaidi huko Namibia na Angola

Idara ya Huduma za Dharura ya UM OCHA, inasema mafuriko yanayotokea huko Namibia na Angola kutokana na mvua kali za wiki tano zilizopita yanahatarisha kueneza magonjwa ya kipindupindu na malaria.

Siku ya kimataifa ya kukomesha Ubaguzi wa Rangi

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, Navi Pillay amesema mamilioni ya watu kote duniani wanaendelea kua wathirika wa ubaguzi wa rangi na kikabila.

Utawala na uthabiti unaanza kurudi Somalia asema Mjumbe Maalum wa UM

Akiliarifu Baraza la Usalama juu ya hatua za kuchukuliwa katika kutekeleza makubaliano ya Djibuti, huko Somalia, Mjumbe Maalum wa UM amesema utawala wa kisheria umeanza kurudi huko Mogadishu, kukiwepo na serekali na taasisi za utawala zinazo tambuliwa kikanda, kimataifa na idadi kubwa ya wa-Somali.

UNHCR inasema mashambulio mepya ya waasi ya wakimbiza raia DRC

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la UM UNHCR limetangaza Ijumaa kwamba mashambulio yanayofanywa na waasi wa kihutu kutoka Rwanda yanaendelea kusababisha watu kukimbia makazi yao huko mashariki ya JKK.

Haki za Binadamu za zorota DRC

Mapema wiki hii naibu Kamishna wa Haki za Binadamu Kyung-wha Kang ameliambia Baraza la haki za Binadamu mjini Geneva ingawa dunia nzima imekua ikizingatia juu ya ugomvi katika eneo la mashariki lenye ghasia huko JKK, ukiukaji wa haki za binadamu umekua ukitokea katika sehemu nyenginezo za taifa hilo kubwa la Afrika.