Afrika

Ushirikiano mpya wa Finland na UM kulinda misitu

Shirika la Chakula na Kilimo FAO na serekali ya Finland zimezindua mpango mpya wa miaka minne, utakaogharimu dola milioni 14 kwa lengo la kusiadia nchi zinazoendelea kulinda rasilmali yao ya misitu na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

UNHCR - Wasomali wazidi kukimbilia Kenya

Maelfu ya wa Somali wanaendelea kukimbilia kaskazini mashariki ya Kenya kutafuta hifadhi katika makambi ya wakimbizi yaliyofurika watu ya Dadaab, licha ya kuwepo na serekali mpya Mogadishu na kupunguka kwa ghasia nchini humo.

AU-UM wasafirisha vifaa vya mtihani kwa wanafunzi Darfur

Afisi ya pamoja ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika AU na UM huko Darfur UNAMID imesaidia hii leo kusafirisha kwa ndege vifaa vya mtihani kwa shule za secondary za maeneo ya mbali katika jimbo hilo la magharibi ya Sudan linalokumbwa na ghasia.

ILO yasisitiza haja ya kubuniwa ajira wakati wa kufufua uchumi

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani ILO amezihimiza serekali za dunia kulenga mipango yao ya kuokoa uchumi katika tatizo la muda mrefu linaloendelea, la ukosefu ajira.

IOM, UNHCR, watoa chombo kuwaelimisha wahamiaji wepya ulaya

Katika juhudi za kuwaelimisha wahamiaji wepya wanaoingia nchi za Umoja wa Ulaya EU, Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi UNHCR, likishirikiana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM, na msaada kutoka EU wamezindua hii leo chombo kipya chenye jina la "Not Just Numbers" siyo takwimu pekee.

UM kuwasaidia wapiganaji wa zamani Sudan kurudi maisha ya kawaida

Zaidi ya wapiganaji wa zamani 180 000 katika vita vya zaidi ya miongo miwili vya wenyewe kwa wenyewe kati ya kaskazini na kusini huko Sudan, watasaidiwa kurudi katika maisha ya kawaida, wakati zowezi la kuwapokonya silaha inaingia awmu mpya.

Vijana wa mjini kupata msaada kutoka mpango mpya wa UM

Kutokana na hali kwamba karibu robo tatu ya wakazi bilioni moja wa dunia wanaoishi kwenye vitongoji vya ufukara ni vijana chini ya miaka 30, shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa limeanzisha mradi mpya wa kuwezesha makundi ya kijami yanayongozwa na vijana.

Hatua za kuimarisha chakula Benin zapongezwa na mtaalamu wa UM

Mtaalamu wa UM juu ya haki ya kupata chakula, Olivier De Schutter amepongeza juhudi za Benin kuimarisha usalama wa chakula huku akisisitiza kwamba juhudi hizo zinabidi pia kuimarisha hali ya maisha ya wakazi maskini.

KM atoa mwito wa kuachiwa wafanyakazi wa UM

KM Ban Ki-moon, akiungana pamoja na wafanyakazi wengine wa UM wametoa mwito hii leo kuachiliwa huru wafanyakazi 19 wa UM wanaoshikiliwa au hawajulikani walipo kote duniani.

China kusaidia mataifa yanayoendelea katika kilimo

Shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO, limesema kwamba China imeingia katika jumuia ya wafadhili wa kuu wa shirika hilo, kwa kutoa dola milioni 30 kuanzisha fuko maalumu la kuimarisha uzalishaji chakula katika nchi zinazoendelea.