Afrika

Wapiganaji watoto Darfur wameanza kupokonywa silaha na UM

Watoto 36 waliohusiana na makundi yenye silaha katika mji wa Tora, Darfur Kaskazini, wameripotiwa na UM kwamba Ijumapili walipokonywa silaha na mashirika ya kimataifa, na baadaye kurudishwa makwao.

Mashirika ya kimataifa yameandaa mradi wa kutoa hadhari za mapema dhidi ya miripuko ya moto

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo (FAO) likijumuika na Shirika la Ulaya juu ya Anga Nje ya Dunia (ESA), pamoja na Shirika la Marekani Linalosimamia Uchunguzi wa Anga (NASA) yameripoti juu ya umuhimu wa kudhibiti haraka miripuko ya moto ilioshuhudiwa kutukia ulimwenguni katika siku za karibuni, kwenye sehemu mbalimbali za dunia, hasa yale maeneo ya karibu na Bahari ya Mediterranean, kusini ya Jangwa la Sahara, Australia na katika Amerika ya Kaskazini.

Machafuko ya makazi bora Afrika Kusini yanaitia wasiwasi UN-HABITAT

Shirika la UM juu ya Makazi (UN-HABITAT) limeripoti kuingiwa na wasiwasi kuhusu maandamano ya machafuko yaliozuka majuzi kwenye vitongoji vya Afrika Kusini, ambapo mamia ya watu walidai wapatiwe makazi madhubuti ya nyumba, pamoja na kupatiwa huduma za maji safi ya kunywa, umeme na mazingira yalio safi.

Mjumbe wa UM ameyakaribisha mazungumzo ya Kamati ya JSC juu ya usalama Usomali

Imetangazwa hii leo kwamba Mjumbe Maalumu wa KM kwa Usomali, Ahmedou Ould-Abdallah, amekaribisha ule mkusanyiko wa wajumbe wa ile Kamati ya Pamoja juu ya Usalama (JSC) uliotukia kwenye mji wa Mogadishu Ijumamosi, mnamo tarehe 25 Julai (2009).

Ban ausihi ulimwengu ujirekibishe kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

KM Ban Ki-moon, kwenye hotuba alioitoa Ulaanbaatar, mji mkuu wa Mongolia Ijumatatu ya leo, kuhusu "Marekibisho ya Kudhibiti Athari za Mabadiliko ya Hali ya Hewa Duniani" alieleza kwamba nchi zilizozungukwa na bara husumbuliwa sana na vizingiti vinavyokwamisha juhudi za kusukuma mbele maendeleo yao, hususan katika kipindi ambacho nchi hizi zisio na pwani huwa zinaathirika pia kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa,

KM ameteua Kamanda Mkuu mpya wa UNAMID kutoka Rwanda

KM amewaariifu wajumbe wa Baraza la Usalama kwamba kutokana na maafikiano na Mwenyekiti wa Kamisheni ya UA, wamemteua Liuteni Jenerali Patrick Nyamvumba wa Rwanda kuwa Kamanda Mkuu mpya wa Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID), kuanzia tarehe mosi Septemba, mwaka huu.

Taarifa rekibisho ya maambuziki ya A/H1N1 kutoka WHO

[Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti Ijumaa, kutokea Geneva kwamba maambukizi ya homa ya mafua ya A/H1N1 bado yanaendelea kimataifa, hali ambayo imeshasababisha vifo vya wagonjwa 800 katika nchi 160 duniani, zilizoripoti kugundua maambukizi ya maradhi haya kwenye maeneo yao.

Ban anaamini miradi ya kudhibiti uchafuzi wa hali ya hewa Uchina inaweza kurudiwa kimataifa

KM Ban Ki-moon, ambaye anafanya ziara ya siku nne katika Uchina, Ijumaa alihudhuria mjini Beijing, tukio la kuanzisha mradi bia wa UM na Serikali ya Uchina kuhimiza umma wa huko, kutumia ile balbu ya taa yenye kuhifadhi nishati na inayotumika kwa muda mrefu.

Suluhu ya kikanda Afrika ndio yenye uwezo wa kukomesha mizozo, inasema BK

Baraza Kuu (BK) Alkhamisi limepitisha, bila kupingwa, azimio liliobainisha umuhimu wa kutumia utaratibu wa kikanda kuzuia na kusuluhisha mizozo katika bara la Afrika.

Msomi wa Kenya, Ngugi wa Thiong'o, ajumuisha maoni binafsi juu ya 'wajibu wa kimataifa kulinda pamoja raia'

Alkhamisi asubuhi, kwenye kikao cha Baraza Kuu, kisio rasmi, walikusanyika wataalamu wa kimataifa walioshiriki kwenye majadiliano yenye hamasa kuu, kuzingatia ile rai ya miaka ya nyuma ya kukomesha kile kilichotafsiriwa na wajumbe wa UM kama ni "kiharusi cha kimataifa" katika kukabili maovu na ukatili unaofanyiwa raia, ndani ya taifa, wakati wenye mamlaka wanaposhindwa kuwapatia raia hawa ulinzi na hifadhi wanayostahiki.