Ili kuudhibiti ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona, serikali ya Uganda imeamua kushirikiana zaidi na wadau mbalimbali yakiwemo makampuni ya mawasiliano na yale ya vinywaji katika juhudi za kuimarisha chanjo. Je, kampeni hiyo inatekelezwaje? Na mtazamo wa Waganda kuhusu chanjo hiyo ukoje sasa? Hii hapa taarifa iliyoandaliwa na mwandishi wetu wa Uganda John Kibego.