Afrika

Mambo 5 ya kufahamu kuhusu mkutano wa Bahari wa UN, fursa ya kuokoa mfumo mkubwa kabisa wa ikolojia 

Bahari ndiyo mfumo mkubwa zaidi wa ikolojia wa sayari dunia, unaodhibiti hali ya hewa, na kutoa uwezo wa maisha kwa mabilioni ya watu.  

Mlinda amani kutoka Guinea auawa nchini Mali

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio la bomu lililofanywa leo mjini Kidal  nchini Mali dhidi ya msafara wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kuleta Utulivu nchini Mali (MINUSMA). Msafara huo ulikuwa kwenye operesheni ya kusaka na kugundua mabomu.

Mataifa yaliyoendelea toeni fursa zaidi kwa wakimbizi.

Kuelekea siku ya wakimbizi duniani tarehe 20 juni, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameyahimiza mataifa yaliyoendelea duniani kutoa fursa zaidi kwa wakimbizi wanaosaka makazi mapya.

Hivi ndivyo tunavyopaswa kusaidia wathaarika wa unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya vita

Unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya vita ni moja ya mbinu ya kivita na ukandamizaji ambayo imeathiri idadi kubwa ya watu, kuharibu maisha yao na kuvunja jamii kwakuwa waathirika wa unyanyasaji huo hubeba mzigo mkubwa wa unyanyapaa, kuathirika kisaikolojia na mara nyingi jamii kuwatupia lawama huku wahalifu mara chache huchukuliwa hatua kwa matendo yao.

Ndui ya Nyani au Monekypox imesambaa katika nchi 42

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO limesema tangu tarehe 1 Januari 2022, wagonjwa wa ndui ya nyani au  Monkeypox wameripotiwa kutoka Mataifa 42 Wanachama katika kutoka mabara matano ya WHO (Amerika, Afrika, Ulaya, Mediterania ya Mashariki na Pasifiki ya Magharibi).

Kauli za chuki ni hatari kwa kila mtu: Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kauli za chuki ni hatari kwa watu wote na kila mtu anao wajibu wakuzuia kauli hizo katika jamii.

Dunia inapotea kwa kujikita katika matumizi ya mafuta kisukuku aonya Guterres 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya kwamba mwenendo wa sasa wa uchumi wa dunia ambao unajikita zaidi katika matumizi ya rasilimali kama mafuta kisukuku utaongeza zahma ya mfumuko wa bei, changamoto ya mabadiliko ya tabianchi na vita. 

Chonde chonde ongezeni fedha tunusuru wakimbizi Burkina Faso- UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR lina hofu kubwa juu ya ongezeko la mashambulizi na ghasia vinavyofanywa na makundi yalioyjihami dhidi ya raia nchini Burkina Faso.

Mtazamo kuhusu afya ya akili, hatua na matibabu vibadilike – WHO

Mwelekeo wa afya ya akili duniani  unazidi kutia shaka na shuku na Umoja wa Mataifa umetoa ripoti ya kutaka watoa maamuzi na wachechemuzi kuhusu afya ya akili waongeze bidii ili kubadili mtazamo wa watu, tiba na hatua dhidi ya chanzo cha tatizo la afya ya akili, matibabu na huduma.
 

Gambia: Miongo minne ya kutumia ngoma kuhamasisha chanjo kwa jamii 

Utoaji wa chanjo kwa watoto umekuwa unakumbwa na changamoto katika baadhi ya maeneo duniani kutokana na jamii kuwa na imani potofu na ndio maana huko nchini Gambia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limeamua kutumia washawishi kwenye jamii ili kuhamasisha wazazi kupeleka watoto wao kupata chanjo.