Huko Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wasanii vijana wanatumia sanaa ya upakaji kuta rangi kama njia mojawapo ya kuhamasisha jamii kuachana na ghasia sambamba na kueneza kauli za chuki.
Njaa inazidi kuwazonga zaidi ya waethiopia milioni 20 ambao wanakabiliwa na vita kaskazini mwa nchi hiyo, ukame katika eneo la kusini na kupungua kwa msaada wa chakula na lishe kuanzia mwezi ujao, limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP
Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kukabiliana na madawa ya kulevya na uhalifu UNODC imesema mfumo mbadala wa kutimiza na kusaka haki na sheria umeanza kuzaa matunda nchini Kenya.
Takriban Watoto milioni 8m walio na umri wa chini ya miaka 5 katika nchi 15 zinazokabiliwa na majanga wako katika hatari ya kifo kutokana na uzito mdogo kupindukia endapo hawatapata haraka matibabu ya lishe na huduma zinazotakiwa limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.
Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa hii leo yamesema kuwa ingawa idadi ya shule zisizo na huduma za msingi za maji na kujisafi, WASH zimepungua bado kuna pengo kubwa la huduma hizo ndani ya nchi n ahata baina ya nchi.
Maelfu ya watu yaaminika wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu huko Kaskazini mwa Chad kufuatia mapigano kati ya wachimba madini ya dhahabu kwenye jimbo la Tibesti karibu na mpaka na Libya.
Wakati hii leo dunia ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya Utumishi wa Umma, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema siku hii isitumike kusherehekea pekee watumishi wa umma duniani kote bali pia kujitoa kwao kufanya kazi kwa ushirikiano ili kujenga Maisha bora ya baadae ya watu wote.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI, UNAIDS limeshukuru mataifa yaliyoanza kuongeza fedha za ufadhili kwa ajili ya shughuli za uwekezaji ili kumaliza UKIMWI duniani.
Mabadiliko ya tabianchi yanaleta madhara kila kona ya dunia ikiwemo kupungua kwa viwango vya mvua na hivyo kuleta usumbufu mkubwa wa wakulima, mathalan nchini Mauritani kiwango cha mvua kilichokuwa kikinyesha miaka 30 iliyopita sasa wanapata robo tu ya kiwango hicho hali iliyowatesa wakulima na wafugaji lakini mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya kilimo IFAD umewanusuru kwa kuwahakikishia maji mwaka mzima.
Kasi ya kutengeneza aina mpya ya dawa za kuua vimelea au bakteria ni ndogo mno kiasi kwamba haitoshelezi kukabiliana na ongezeko la usugu wa dawa hizo zijulikanazo pia kama viuavijasumu.