Afrika

UNICEF kuwachanja watoto Rwanda

Wizara ya afya ya Rwanda ikisaidiwa na shirika la Watoto la UM, UNICEF, imezindua kampeni ya pili ya wiki moja, kuwahi kufanywa nchini humo ya kuwapatia kinga watoto na kina mama kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuiliwa kwa urahisi.

Watu saba wapoteza maisha katika ajali nje pwani ya Yemen.

Kiasi ya wahamiaji saba wa Kiafrika walizama na kufariki mwishoni mwa wiki wakati meli ya biashara ya magendo walokua wanasafiria ilipozama muda mfupi tu baada ya kutia n\'ganga kwenye bandari ya Aden huko Yemen.

Mjumbe maalum apongeza mkataba na waasi huko DRC

Mjumbe maalum wa UM huko JKK amesifu makubaliano yaliyotiwa sahihi Ijumatatu kati ya serekali ya Kinshasa na kundi la waasi lililokua likiendesha mapigano yaliyosababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao huko mashariki ya nchi mwaka jana.

Ban anasema kiwango cha uwambukizaji wa kifua kikuu kinapungulia

Akiadhimisha siku ya kifua kikuu duniani hii leo, KM Ban Ki-moon amesema kasi za kupungua ugonjwa wa kifua kikuu zinakwenda pole pole na kuonya kua juhudi za kupambana na ugonjwa huo zinapunguka.

Rais wa Sudan atembelea Eritrea bila ya kukamatwa

Rais Omar Al-Bashir wa Sudan amabae amefunguliwa mashtaka na Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa, ICC, alipokelewa na kiongozi mwenzake Isaias Afwerki wa Eritrea na wananchi, licha ya kwamba kuna hati ya kimataifa ya kukamatwa kwake.

Pendekezo la FAO la Mkutano wa Viongozi juu ya Mzozo wa Chakula lapata Nguvu

Shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO, limesema kwamba pendekezo la kuitisha mkutano wa viongozi duniani mwishoni mwaka 2009 juu ya mzozo wa chakula, ambao unazidi kuzorota katika nchi maskini, linapata nguvu na kupewa umuhimu mkubwa.

UM yaadhimisha Siku ya Utabiri wa Hali ya Hewa

Ikiadhimisha siku ya Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani leo Jumatatu, Idara ya UM ya kutabiri hali ya hewa WMO, inazingatia juu ya uchafuzi wa hewa duniani, kutokana na takwimu kwamba, kiasi ya watu milioni mbili duniani hufariki mapema kutokana na hewa chafu kila mwaka.

Ban anapongeza kuachiliwa mfanyakazi moja wa UM huko Niger

KM Ban Ki-moon amepongeza hii leo kauchiliwa huru mfanaykazi mmoja wa UM aliyetekwa nyara Niger mwishoni mwa mwaka jana na akarudia tena mwito wake wa kuachiliwa huru wafanyakazi wengine wawili pamoja na mwakilishi wa UM nchini humo, Robert Fowler kutoka Canada.

KM anasema ni lazima dunia kufanya kazi pamoja kutumia maji kwa busara

KM wa UM Ban Ki-moon amesisitisza umuhimu wa maji kama nguvu za kungana pamoja kuliko kiungo cha mizozo, akihimiza kwamba mustakbala wa pamoja wa dunia unategemea jinsi inavyosimamia rasilmali yake hii tunu.

Mahojiano na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, na Watoto, ya Tanzania Bi. Mariam Joy Mwaffisi

Wajumbe kwenye mkutano wa Kamisheni juu ya Hali ya Wanawake walijadili kwa mapana marefu namna ya kuhamasisha haja ya wanawake na wanaume kufanya kazi pamoja katika majukumu ya malezi, kuwahudumia waathiriwa wa HIV na Ukimwi, pamoja na majukumu ya nyumbani.