Afrika

Wasi wasi wazidi huko Madagascar baada ya mkutano kutofanyika tena

Mkutano ulopangwa kufanyika kati ya pande zinazogombana huko Madagascar haukuweza kufanyika tena hii leo baada ya meya wa Antananarivo, Andry Rajoelina kukata kuhudhuria mazungumzo.

Dola milion 50 za Marekani kuimarisha haki za wanawake UNFPA

Rais Barack Obama, wa Marekani ametoa dola milioni 50 kusaidia shirika la wakazi la UM UNFPA, ili kupunguza umaskini na kuimarisha afya ya wanawake na watoto katika zaidi ya mataifa 150.

KM Ban ana wasi wasi kutokana na kutekwa wafanyakazi wa msaada Darfur

KM Ban Ki-moon ameeleza wasi wasi wake hii leo kutokana na kutekewa nyara wafanyakazi watatu wa huduma za dharura huko Darfur, na kwa mara nyingine tena alitoa mwito kwa Serekali ya Sudan kubadili uwamuzi wake wa wiki iliyopita, wa kuyafukuza makundi 13 muhimu ya misaada.

Mazungumzo kuzihusisha pande zote Afrika ya Kati kutapelekea amani

Mjumbe Maalum wa KM kwa ajili ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, ameliambia Baraza la Usalama kwamba mazungumzo yaliyokua yanasubiriwa kwa muda mrefu ya vyama vyote yameweza kuleta nafasi ya kupiga hatua kuelekea amani ya kudumu katika nchi hiyo isiyopakana na bahari.

Wataalamu wamulika athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa afya

Athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa afya, ni suala muhimu ambalo wapanga sera wanabidi kuzingatia na kufahamu wanapopanga vipau mbele vya maendeleo na uwekezaji.

KM Ban na Rais Obama wajadili kuimarisha uhusiano kati ya UM na Marekani

KM Ban Ki-moon na Rais Barrack Obama wa Marekani wamekubaliana juu ya umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Marekani na UM walipokutana Ijumanne huko Washington.

Hapa na pale

Idara ya UM ya kupambana na mabomu yaliyotegwa ardhini, UNMAS imetangaza kwamba serekali ya Japan itatowa karibu dola milioni 7.7 ya msaada kwa ajili ya juhudi za kuondowa mabomu yaliyotegwa ardhini huko JKK na Chad.

Kesi mpya za kutoweka zaidi ya watu 300 kushughulikiwa na tume ya UM

Kamati ya UM ya kufuatilia kutoweka kwa nguvu au kwa hiyari watu, ina mpango wa kutathmini kesi mpya za kutoweka watu wengine 326 zilizowasilishwa na habari mpya kutoka nchi 32 za dunia wakati wa kikao cha kwanza kati ya tatu ya mkutano wamwaka wiki hii.

Kuporomoka kwa biashara duniani kunaweza kuathiri zaidi wanawake

Akifungua mkutano juu ya "umuhimu wa jinsia katika biashara" mkurugenzi mkuu wa shirika la Biashara Duniani UNCTAD Bw Supachai Panitchpakdi amezipendekeza serekali zinazo tayarisha mipango ya kujaribu kuufufua uchumi ili kukabiliana na mzozo wa kifedha duniani kufikiria juu ya kuweka hatua za kuimarisha ajira kwa ajili ya wanawake na kusaidia biashara ndogo ndogo zinazoendeshwa na wanawake.

Walinda amani wa UNAMID wavamiwa kwa ghafla huko Darfur

Ujumbe wa pamoja wa walinda amani wa UM na Umoja wa Afrika, UNAMID huko Sudan Magharibi, umesema walinda amani walivamiwa kwa ghafla na watu watano au sita waliokuwa na silaha Jumatatu jioni, wakati wakisafiri kwa gari karibu na mji wa EL- Geneina huko darfur magharibi.