Afrika

Kongamano la 11 la mijini duniani limeng’oa nanga Katowice, Poland:UNHABITAT

Kikao cha kumi na moja cha Kongamano la kimataifa la miji endeleu kimefunguliwa rasmi leo Katowice, Poland kwa wito wa kuongeza juhudi maradufu ili kukabiliana na changamoto zinazoletwa mijini na janga la COVID-19, dharura ya mabadiliko ya tabianchi na migogoro.

Vijana ni kizazi kitakachosaidia kuokoa bahari na mustakbali wetu:Guterres

Dunia lazima ifanye jitihada zaidi ili kukomesha kuzorota kwa hali ya afya ya bahari, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo Jumapili, akiwataka vijana waliokusanyika Carcavelos, Ureno, kwa ajili ya jukwaa la vijana na ubunifu la Umoja wa Mataifa kuongeza kasi kwa sababu viongozi wa kizazi chake wanasuasua.

Hatuwezi kuruhusu tatizo la mihadarati kuendelea kuathiri mamilioni ya watu:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema siku ya kimataifa ya ya kupambana na matumizi mabaya ya dawa za kulevya na usafirishaji haramu ya mwaka huu inaangazia athari za changamoto za dawa za kulevya katika majanga ya kiafya na kibinadamu.

Watesaji wasiruhusiwe kukwepa sheria kwa uhalifu wao:UN

Katika siku ya kimataifa ya kusaidia waathirika wa utesaji Umoja wa Mataifa unataka hatua Madhubuti zichukuliwe ili kuhakikisha watesaji wanahukumiwa kutokana na uhalifu huo.

Monkeypox ni tishio lakini si dharura ya afya ya umma inayoleta hofu ya kimataifa: WHO

Ingawa mlipuko wan dui ya nyani au monkeypox unaendelea na umeshasambaa katika mataifa kadhaa ulimwenguni mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema “Nina wasiwasi mkubwa na kusambaa kwa mlipuko wa monkeypox ambao ni tishio linaloendelea, nimeitisha kikao cha kamati ya dharura ya WHO, na wataalam wameshauri kwamba kwa sasa ugonjwa huo sio dharura ya afya ya umma inayotia hofu ya kimataifa.”

WHO yakaribisha dola milioni 250 kutoka Novartis kukabili magonjwa ya NTDs na malaria

Shirika la afya la Umoja wa Mataiofa duniani WHO leo limekaribisha tangazo kwamba shirika la dawa la Novartis litatoa dola za milioni 250 kwa ajili ya mapambano dhidi ya magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika (NTDs) na malaria.

Dunia inawategemea sana mabaharia, lazima tuwathamini:Guterres

Mchango wa mabaharia haupimiki nani muhimu sana kwa watu na maendeleo yao, kwani dunia inawategemea sana amesem Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Mashirika ya UN yapaza sauti kufuatia uamuzi wa Mahakama Kuu ya Marekani kuhusu utoaji mimba

Iwe utoaji wa mimba ni halali kisheria au si halali kisheria, bado hufanyika mara kwa mara, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi duniani, UNFPA hii leo kupitia taarifa iliyotolewa jijini New York, Marekani.

Rais wa Baraza Kuu la UN, aitumia CHOGM kupeleka ujumbe mzito

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Abdulla Shahid yuko katika mji Mkuu wa Rwanda Kigali ambako unafanyika Mkutano wa 26 wa wakuu wan chi za Jumuiya ya Madola.

Guterres azindua ajenda ya hatua kukabili ukimbizi wa ndani

Dunia yetu inakabiliwa na janga la ukmbizi wa ndani! Ndivyo alivyoanza ujumbe wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ujumbe ambao ametoa leo kwa njia ya video kuzindua ajenda yake ya hatua dhidi ya ukimbizi wa ndani.