Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amepongeza hatua iliyofikiwa nchini Gabon ambayo imewawezesha kundi la watu kadhaa waliokuwa wakipata hifadhi kwenye majengo ya umoja huo kujerea makwao kwa hiari na amani.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amebaini kwa masikitiko na hofu kubwa kwamba helkopta tatu za kivita na vifaa vingine kutoka Belarus vimearifiwa kupelekwa Yamoussoukro kwa ajili ya majeshi ya Laurent Gbagbo.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hilary Clinton akizungumza kwenye mkutano wa baraza la haki za binadamu amesema macho yote hii leo yanajikita kwa Libya.
Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Antonio Guterres ameelezea hofu yake juu ya maelfu ya wakimbizi na raia wa kigeni ambao huenda wamekwama nchini Libya.