Afrika

Benki ya Dunia yaingilia kati kukabili uhaba wa chanjo Afrika

Katika kufanikisha lengo la Muungano wa Afrika, AU kuhakikisha asilimia 60 ya wakazi wa bara lake wamepatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Corona au COVID-19 ifikapo mwaka 2022, Benki ya Dunia na AU wametangaza ubia wa kuunga mkono mpango wa kikosi kazi cha Afrika cha kupata chanjo hizo, AVATT utakaoruhusu nchi za Afrika kununua na kusambaza dozi za chanjo kwa ajli ya watu milioni 400 barani kote.

Kuisaidia WFP ni kuwasaidia wakimbizi kama Adu

Mkimbizi wa ndani Abbas Adu na wengine 400,000 wamelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula WFP kuwapatia msaada wa chakula wakati huu ambapo WFP imepaza sauti kwa wahisani kusaidia wananchi Milioni 41 wanaokabiliwa na njaa kutokana na hali mbaya ya hewa ambayo imeathiri mavuno yao na hivyo kukosa chakula.

Amani ni rasilimali adimu ambayo wengi wanaililia:Muhudumu wa kujitolea Gbambi

Kutana na mfanyakazi wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Jason William Gbambi ambaye anafanyakazi kama afisa uhamasishaji wa timu ya maadili na nidhamu ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS. Anasema kufanyakazi ya kujitolea ni kukumbatia jamii na kutambua mahitaji yao na hasa amani ambayo ni adumu nchini humo. Flora Nducha na taarifa zaidi 

Muongo mmoja wa Uhuru Sudan Kusini bado usalama unasuasua

Taifa changa zaidi duniani Sudan Kusini linaenda kutimiza muongo mmoja tangu kupata uhuru wake lakini Umoja wa Mataifa unasema bado kuna kazi kubwa ya kufanya kwani baadhi ya makubaliano hayatekelezwa, watu wenye nia ovu wanaendelea kuwatesa raia na wafanyakazi wa mashirika ya misaada nao wanavamiwa na kuuawa. 

Watoto hawapaswi kuwa kipaumbele cha mwisho cha ajenda ya kimataifa – Virginia Gamba 

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto kwenye mizozo ya kivita Virginia Gamba amesema inasikitisha kuona ripoti ya mwaka kuhusu watoto na mizozo ya silaha inachapishwa katika kipindi ambacho bado kuna mateso makali kwa watoto katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.

Je wafahamu vinavyotibua bayonuai?

Muongo wa kurejesha bayonuai umezinduliwa rasmi mwezi huu wa Juni mwaka 2021 kwa lengo la kurekebisha kile ambacho mwanadamu amefanya kuharibu mazingira ya sayari dunia na vile vile kuchukua hatua kuepusha uharibifu. Je nini kinaharibu bayonuai? Lucy Igogo wa kituo cha habari cha  Umoja wa Mataifa UNIC jijini Dar es salaam nchini Tanzania amezungumza na Clara Makenya, Mwakilishi wa shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP nchini humo. Bi. Makenya anaanza kwa kuelezea chanzo cha muongo huo.

Idadi ya wanaojifungua kwa njia ya upasuaji usio wa lazima inaongezeka:WHO 

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO inasema kiwango cha wanawake kujifungua kwa njia ya upasuaji kinaongezeka duniani kwa idadi inayoashiria taratibu zisizo za lazima za kiafya na zinazoweza kuletya madhara. Flora nducha amefuatilia ripoti hiyo na kuandaa taarifa hii 

Asilimia 99 ya Watoto Niger hawajui kusoma na kuandika:Benki ya Dunia

Ikiwa leo ni siku ya mtoto wa Afrika, ndoto za kutimiza ajenda ya bara hilo ya mwaka 2040 ya kuwa na bara la Afrika linalomfaa mtoto wa Afrika ikiwemo katika suala la kupata elimu, kwa Niger huenda lisitimie kwani asilimia 99 ya watoto wenye umri wa miaka 10 ni wajinga wa kutokujua kusoma na kuandika.

 

Teknolojia imetuokoa wakati wa COVID-19 kusaidia jamaa nyumbani:DKT.Minja

“Zile fedha ambazo tunazituma zinamchango mkubwa sana sio tu kwa familia hata kwa jamii nzima kwa ujumla kwa maana ya kiuchumi .”  Dkt. Frank Minja 

Utumaji fedha kimtandao ulinusuru familia za kijijini mwaka 2020 

Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD umesema ingawa kiwango cha wahamiaji kutuma fedha nyumbani kimtandao  wakati wa janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 mwaka 2020 kimeongezeka, bado kaya za vijijini zilishindwa kunufaika vyema na utumaji huo kutokana na kukosa miundombinu ya kidijitali ya kupokea fedha hizo. IFAD imesema hayo ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya familia kutumiana fedha.