Afrika

Afrika ni mfano wa kuigwa katika suala la kuhudumia wakimbizi na wahamiaji.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres  hii leo baada ya mkutano wake na mwenyekiti wa Kamisheni ya Muungano wa Afrika, AU mjini Addis Ababa Ethiopia amewaeleza wanahabari kuwa  nchi za Afrika ni mfano kwa nchi tajiri wakati linapokuja suala la kuwahudumia wakimbizi.

Viongozi wa Afrika wanusuruni watoto milioni 13.5 waliofurushwa makwao– UNICEF

Mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Muungano wa Afrika, AU ukianza kesho Jumamosi huko Addis Ababa Ethiopia, takribani Watoto milioni 13.5 barani Afrika wamefurushwa makwao.

Ukosefu wa usawa ukizidi kuota mizizi, UN yahaha kuhakikisha kunakuwepo na usawa

Ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu au SDGs- ni mwongozo wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mustakabali mzuri na endelevu kwa wote- na unatoa wito kwa kuziba pengo la utofauti kati ya nchi na ndani ya nchi. Hatahivyo, ukosefu wa usawa kimataifa unaongezeka. Kwa hiyo ni ni kifanyike?

Mada kwa kina: Kala Jeremiah na matumizi ya nyimbo zake kutetea haki za watoto na vijana

Nchini Tanzania wasanii wanatumia mbinu mbalimbali kusaidia jamii inayowazunguka kwa kutambua kuwa msanii ni kioo cha jamii na hivyo akionacho ndicho ambacho anakiwasilisha kwa jamii yake kwa lengo la kuelimisha au kuburudisha jamii hiyo husika.

Msaada zaidi kwa Tanzania wahitajika ili ihudumie vyema wakimbizi- Grandi

Kamishna Mkuu wa shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa ,UNHCR, Filippo Grandi amehitimisha ziara yake ya siku nne nchini Tanzania akitoa wito kwa jamii ya kimataifa kuwekeza zaidi mikoa ya kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo ambayo ni nyumbani kwa wakimbizi 330,000. 

Waandishi wa habari 400 Afrika Magharibi wamepatiwa mafunzo na IOM

Ripoti sahihi, dhahiri na zilizoandikwa kwa ufasaha kuhusu wahamiaji zina wajibu muhimu wa kuelimi Afrika Magharibi kuhusu uhamiaji wakiholela na katika kuwajumuisha tena kwenye jamii wahamiaji wanaorejea katika jamii zao limesema shirika la kimataifa la uhamiaji IOM.

Lishe bora ni haki ya kila mtoto:UNICEF

Lishe bora na huduma zingine za msingi kama elimu na afya ni haki ya kila mtoto kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, lakini mara nyingi mamilioni ya watoto hukosa haki hiyo hususani lishe bora kutokana na sababu mbalimbali. UNICEF inasema hali hiyo  inaweka afya za watoto hatarini na pia njiapanda mustakhbali wao.

Dau la plastiki latia nanga mji mkongwe Zanzibar

Hatimaye dau la plastiki lililosafiri kilometa 500 kutoka Lamu, nchini Kenya hadi Mji Mkongwe, Zanzibar nchini Tanzania limetia nanga Unguja likiwa limetimiza azma yake ya  kuelimisha jamii zilipo pwani kwa Kenya na Tanzania kuhusu madhara ya plastiki kwa binadamu, mazingira na viumbe vya majini. 

Dola milioni 15 za mfuko wa ‘Elimu haiwezi kusubiri’ zaanza kuleta manufaa kwa wakimbizi wa Sudan Kusini walioko Ethiopia.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Ethiopia linasimamia uwekezaji wa mfuko wa dunia wa dola milioni 15 wa  kufanikisha mpango uliopewa jina ‘Elimu haiwezi kusubiri’wenye lengo la kuinua ubora wa elimu kwa wakimbizi na wenyej nchini humo. 

Makubaliano  ya amani CAR yatiwa saini Bangui, ni baada ya kupitishwa Khatroum, Guterres azungumza

Hii leo  huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, wajumbe wa serikali na vikundi 14 vilivyojihami wametia saini makubaliano ya amani yaliyofikiwa kati ya pande mbili hizo mjini Khartoum nchini Sudan mwishoni mwa wiki iliyopita.