Afrika

Dau la plastiki latia nanga mji mkongwe Zanzibar

Hatimaye dau la plastiki lililosafiri kilometa 500 kutoka Lamu, nchini Kenya hadi Mji Mkongwe, Zanzibar nchini Tanzania limetia nanga Unguja likiwa limetimiza azma yake ya  kuelimisha jamii zilipo pwani kwa Kenya na Tanzania kuhusu madhara ya plastiki kwa binadamu, mazingira na viumbe vya majini. 

Dola milioni 15 za mfuko wa ‘Elimu haiwezi kusubiri’ zaanza kuleta manufaa kwa wakimbizi wa Sudan Kusini walioko Ethiopia.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Ethiopia linasimamia uwekezaji wa mfuko wa dunia wa dola milioni 15 wa  kufanikisha mpango uliopewa jina ‘Elimu haiwezi kusubiri’wenye lengo la kuinua ubora wa elimu kwa wakimbizi na wenyej nchini humo. 

Chukua hatua sasa kutokomeza FGM ifikapo 2030:UN

Wakati wa kuchukua hatua ili kutokomeza ukeketaji  au FGM, ifikapo mwaka 2030 ni sasa . Wito huo wa pamoja umetolewa leo ikiadhimishwa siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji na wakuu  wa mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la idadi ya watu UNFPA, Dkt. Natalia Kanem, lakuhudumia watoto UNICEF, Henrietta Fore na la linaloshughulika na masuala ya wanawake UN Women , Phumzile Mlambo-Ngcuka.

Baba alipofariki dunia ndipo FGM ikawa tishio kwetu, Masanga iliniokoa- Msichana Elizabeth

Kuelekea siku ya kimataifa hapo kesho ya kutokomeza ukeketaji wa watoto wa kike na wasichana duniani, FGM, nchini Tanzania, kituo ambacho ni kimbilio kwa watoto wanaokwepa mila hiyo potofu, kimeendelea kuwaepusha watoto wa kike na wao sasa ni mashuhuda. 

Hatua lazima zichukuliwe dhidi ya uonevu kwa watoto na barubaru mtandaoni:UNICEF

Katika kuadhimisha siku ya usalama wa mtandao wa intaneti hii leo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limetoa wito wa kuchukuliwa hatua kuzuia uonevu na ukatili mtandaoni kwa zaidi ya asilimia 70 ya vijana kote duniani.

Makumi ya maelfu ya wakimbizi kutoka Nigeria wamiminika Cameroon-UNHCR

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR nchini Cameroon, limesema linaendelea kupokea wakimbizi kutoka Nigeria ambao wanakimbilia  Cameroon kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara yanayofanywa na kundi la Boko Haram. UNHCR imesema baadhi yao ni wameshakimbia nchi  yao zaidi ya mara tano hadi kumi kwa sababu hawana njia nyingine zaidi ya kujinusuru ili kusaka usalama

Uchungu wa maumivu ya mwana wamfanya mama atamani angaliugua yeye saratani

Katika maadhimisho ya siku ya saratani duniani hii leo, shirika la afya ulimwenguni WHO limeangazia kwa kina saratani ya shingo ya kizazi huku ikisisitiza umuhimu wa kuchunguzwa, kupokea chanjo ya Human Papiloma Virus, HPV na kutokomeza kabisa saratani ya shingo ya kizazi. 

Sisi tukisameheana, watu watatoka kote duniani na kusema alaa! kumbe Sudan Kusini ni pahala pazuri

Mapema wiki hii mjini Juba Sudan Kusini imefanyika mechi ya mpira wa miguu kwa ajili ya kuhamasisha amani kwa kuwaleta watu pamoja. Chini ya jua kali timu A na B za vijana wa umri wa chini ya miaka 23 zilikwaana katika ushindani mkali kwa lengo la kusambaza ujumbe wa amani na umoja kwa mamia ya mashabiki waliohudhuria.