Afrika

Kituo cha kutibu  Ebola Butembo chashambuliwa, UNICEF yafunguka

 “Nachukizwa na shambulio la hivi karibuni zaidi dhidi ya  kituo cha kutibu Ebola huko Butembo, jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC,” ndivyo ilivyoanza taarifa iliyotolewa jioni ya leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, mjini New York, Marekani.

Mlo wa siku moja tu ni changamoto kwa wakimbizi na wasaka hifadhi Misri.

Shirika  la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR hii leo mjini Geneva Uswisi limesema msaada unaotolewa kwa wakimbizi walioko Misri uko katika wakati mgumu kutokana na kuongezeka kwa wakimbizi wapya huku kukiwa na vyanzo haba vya rasilimali.

Nchini Chad, madarasa ya wasichana pekee yasaidia kupunguza hofu na kuchagiza usawa wa jinsia

Mwalimu amenyanyua mchoro wa msichana barubaru ambaye amegutuka tu na kubaini kuwa amechafua nguo yake kutokana na kupata hedhi ya kwanza akiwa shuleni. Mwalimu huyu anazungumza na wasichana walioko darasani kwenye mji wa Bol nchini Chad.

Ujira mdogo katika sekta ya uvuvi ni mtihani kwa wafanyakazi na familia zao:Mtaalam

Mishahara midogo, mazingira duni ya kazi kwa katika vyombo vya  uvuvi, ufugaji wa samaki na miundo mbinu mibovu ya viwanda vya usindikaji ni vina athari kubwa katika maisha ya kila siku ya wafanyakazi. 

Hongera kwa miaka 100 ya siku ya kuzaliwa Brian Urquhart- Umetendea mema UN

Ikiwa leo ni miaka 100 tangu kuzaliwa Sir. Brian Urquhart, mmoja wa wafanyakazi waanzilishi zaidi wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu Antonio Guterres ameumwagia sifa lukuki ikiwemo utumishi uliotukuka na uliosaidia kujenga misingi ya chombo hicho kilichoundw mwaka 1945 baada ya Vita Vikuu vya Pili vya dunia.

Ukosefu wa usalama Ukanda wa Sahel wafurusha watoto; Shule zilizofungwa zaongezeka maradufu

Kuendelea kwa ukosefu wa usalama kwenye ukanda wa Sahel kumesababisha takribani shule 2000 huko Burkina Faso, Mali na  Niger kufungwa kabisa au kushindwa kutoa elimu kwa wanafunzi mwaka 2018.

Mahakama ya kuhamahama yapeleka haki Malakal, Sudan Kusini.

Kwa zaidi ya kipindi cha siku tatu, mahakama ya kuhamahama inayofadhiliwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, imekuwa katika mji wa Malakal  jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini ili kushughulikia kesi kadhaa zikiwahusisha watu ambao walitenda makossa makubwa yakiwemo kesi mbili za unyanyasaji wa kingono na moja ya unyanganyi kwa kutumia silaha.

Elimu  haiwezi kusubiri wapeleka nuru kwa watoto CAR

Serikali ya Jamhuri  ya Afrika ya Kati, CAR kwa ushirikiano na mradi wa Elimu haiwezi kusubiri, ECW,  leo wamezindua mradi wa miaka mitatu wenye lengo la kuboresha elimu nchini humo kama njia mojawapo ya kunasua watoto wa kike na wa kiume kutoka athari za mzozo ulioacha karibu watoto 500,000 bila ya shule.

Mamilioni wanufaika na muamko wa kutokomeza kutokuwa na utaifa Afrika Magharibi-UNHCR

Mamilioni ya watu wamekwepa kutokuwa na utaifa Afrika Magharibi kufuatia mataifa mengi kudhamiria kuhakikisha kuwa kila mtu anapata utaifa ifikapo mwaka 2024 kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.

Dira 2020 ya kunyamazisha silaha Afrika yapatiwa ari mpya na azimio la UN

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limepitisha azimio lenye lengo la kufanikisha suala la kunyamazisha silaha barani Afrika, kwa kuzingatia kuwa mizozo inayorindima katika maeneo mbalimbali kwenye eneo hilo imekuwa kikwazo katika kufanikisha amani, usalama na maendeleo endelevu barani humo.