Afrika

Mkutano wa WCC unazingatia utaratibu mpya wa kueneza taarifa za hali ya hewa kote duniani

Mkutano Mkuu wa Dunia juu ya Hali ya Hewa (WCC-3) umefunguliwa rasmi Geneva Ijumatatu ya leo, ambapo wataalamu na wanasiasa kutoka sehemu mbalimbali za ulimwengu, wanakutana kwa mashauriano ya kuhakikisha umma wa kimataifa huwa unapatiwa uwezo wa kutabiri hali ya hewa pamoja na taarifa nyengine kama hizo, ili kukabiliana vyema na taathira za mabadiliko ya hali ya hewa.

UNAMID imepokea maofisa polisi ziada kutoka Nepal na Nigeria

Shirika la Vikosi vya Mchanganyiko vya UM-UA kwa Darfur (UNAMID) limepokea maofisa wa polisi 26 kutoka Nepal na polisi 30 wa Nigeria waliowasili kwenye mji wa El Fasher leo Ijumatatu.

Umma wa Dungu watishwa kila siku na mashambulio ya LRA, anasema Mkuu wa UNICEF

Ann Veneman, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) kwenye siku ya mwisho ya ziara ya siku tano alioendeleza katika JKK alipata fursa ya kukutana na wale watoto waliotoroshwa na waasi wa Uganda wa kundi la LRA.

Mtetezi wa Haki za Binadamu aisihi Zambia kwamba "ufukara hauondoshwi na ufasaha wa lugha bali vitendo"

Baada ya kukamilisha ziara yake katika Zambia, Mtaalamu Huru wa UM anayetetea haki za binadamu na umaskini uliovuka mipaka, Magdalena Sepúlveda, kwenye mahojiano na waandishi habari mjini Lusaka alionya kwamba "ufukara mkubwa uliopamba nchini Zambia haotofanikiwa kukomeshwa kwa ufasaha wa usemaji bali kwa vitendo halisi."

Taarifa juu ya hali ya maambukizi ya A/H1N1 katika dunia

Shirika la Afya Duniani (WHO) kwenye taarifa ya wiki kuhusu hali ya maambukizo ya homa ya mafua ya A/H1N1 llimeeleza ya kwamba katika nchi za kizio cha kusini ya dunia, ikijumlisha Chile, Argentina, New Zealand na Australia maambukizo ya maradhi yameshapita kilele na hivi sasa yameselelea kwenye kigezo wastani, wakati mataifa ya Afrika Kusini na Bolivia yanaendelea kukabiliwa na ongezeko la homa ya mafua.

Kituo cha kuwasaidia wahamiaji jirani kupata ajira chafunguliwa mpakani Afrika Kusini: IOM

Shirika la Kimataifa juu ya Wahamaji (IOM) limetangaza kufunguliwa Kituo cha Wahamaji wa Ajira katika Afrika Kusini, kwenye mji wa mipakani wa Beitbridge.

Siku 100 zimesalia kabla ya Mkutano wa COP-15 kudhibiti taathira za mabadiliko ya hali ya hewa

UM umetoa mwito maalumu wenye kuwataka mamilioni ya umma wa kimataifa kutia sahihi zao, kwenye mtandao, ili kuidhinisha lile ombi la kuzihimiza serikali wanachama Kukamilisha Makubaliano juu ya waraka wa Mkutano wa COP-15, yaani ule Mkutano Mkuu utakaofanyika mwezi Disemba katika mji wa Copenhagen, Denmark kuzingatia mkataba mpya wa udhibiti bora wa mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni.

Vurugu la waasi wa LRA lasabibisha raia 125,000 ziada kuhama makazi katika JKK

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) limeripoti kutoka Geneva, kwamba kundi la waasi wa Uganda, wanaojiita Jeshi la Upinzani la MUngu (Lord Resistance Army/LRA) bado wanaendeleza, kwa kiwango kikubwa vitendo vya ufisadi, uharibifu na kusababisha uhamisho uliovuka mipaka wa watu katika eneo la mashariki la JKK.

Ofisa wa UNHCR anasailia mzozo wa makazi kwenye kambi za wahamiaji za Dadaab, Kenya

Katika miezi ya karibuni, vurugu na mizozo ya kihali ilikithiri kwa wingi katika Usomali, hali iliosababaisha maelfu ya raia kuamua kuhama makwao na kuelekea mataifa jirani kutafuta hifadhi na usalama.

Wajumbe wa Mkutano wa Kupunguza Silaha wajitahidi kufikia mapatano kwenye mradi wa kazi

Alkhamisi, wajumbe wanaohudhuria Mkutano wa Kupunguza Silaha Duniani, unaofanyika Geneva kwa hivi sasa, bado wanaendelea na juhudi za kusuluhisha mvutano juu ya mradi wa kufanya kazi wa kikao hicho.