Afrika

ICC yathibitisha kesi kwa aliyekuwa naibu-raisi wa JKK

Mahakama ya Kimataifa juu ya Makosa ya Jinai ya Halaiki (ICC) imethibitisha kuwa kuna ushahidi wa kuridhisha wa kuanzisha kesi ya kumtuhumu Jean-Pierre Bemba Gombo, aliyekuwa naibu-raisi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (JKK), kwamba alishiriki kwenye makosa ya vita na jinai iliotengua haki za kiutu.

Siku ya Dunia Kupiga Vita Kuenea kwa Jangwa

Tangu 1995 UM unaihishimu tarehe 17 Juni, kila mwaka, kuwa ni Siku ya Kupiga Vita Kuenea Kwa Jangwa. Ripoti za UM juu ya tatizo la kueneza majangwa, kutokana na matumizi badhirifu ya ardhi, inaashiria watu milioni 200 watalazimika kuhama makazi katika mwaka 2050 kutakakosababishwa na mabadiliko ya katika mazingira.

Uadui dhidi ya watumikia misaada ya kiutu Usomali wahatarisha maisha ya watoto na wanawake, imehadharisha UNICEF

Kaimu Mwakilishi wa Shirika la UNICEF kwa Usomali, Hannan Sulieman amenakiliwa akisema, kutokea Nairobi, kuwa "ameudhika sana" na kuongezeka kwa mawimbi mapya ya mashambulio, uchokozi na uadui uliotanda siku za karibuni, dhidi ya wafanyakazi wanaohudumia misaada ya kiutu katika Usomali.

UNIDO na kampuni ya HP wafungua vituo vya mafunzo katika Afrika na Mashariki ya Kati

Shirika la UM juu ya Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) ikishirikiana na kampuni ya teknolojiya ijulikanayo kama HP, yametangaza kufungua vituo 20 vya mafunzo katika Afrika na Mashariki ya Kati, vitavyotumiwa kuilimisha vijana wa umri wa baina ya miaka 16 mpaka 25, mafunzo yanayohusika na ujasiriamali na teknolojiya ya mawasiliano ya kisasa.

'Afya bora ndio msingi wa kufikia MDGs', asihi KM

Risala ya KM kufunga warsha maalumu kuhusu Afya ya Kimataifa kwenye mazingira ya mizozo, iliotolewa Ijumatano, ilisisitiza kwamba uwezo wa jumuiya ya kimataifa kuyafikilia, kwa wakati, yale Malengo ya Maendeleo ya Milenia, (MDGs) unafungamana kimsingi na matokeo mazuri kwenye zile juhudi za kuendeleza afya ya jamii.

Siku ya Kimataifa kwa Mtoto wa Afrika

Tarehe ya leo, Juni 16, inaadhimishwa na UM kuwa ni "Siku ya Kimataifa kwa Mtoto wa Afrika." Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo kwa Watoto (UNICEF) limetangaza ya kuwa kuna baadhi ya nchi katika Afrika, zilizoonyesha maendeleo makubwa ya kutia moyo, kwenye zile juhudi za kuhudumia watoto wachanga kuishi.

'Watu milioni 42 waling'olewa makwao duniani 2008': UNHCR

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR) leo imewasilisha ripoti ya mwaka ambapo imeeleza idadi ya watu waliolazimika kuyahama mastakimu, kwa sababu ya mateso, fujo na vurugu ulimwenguni, mnamo mwisho wa 2008, ilifikia wahamiaji milioni 42.

Nusu ya vifo vya barabarani huathiri wenda kwa miguu, wapanda baiskeli na wanaoendesha motosekli/pikipiki

Utafiti mpya uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) umethibitisha ya kuwa nusu ya watu milioni 1.27 wanaokadiriwa kufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, ni watu wanaokwenda kwa miguu, na wale wanaopanda baiskeli na wanaoendesha motosekli/pikipiki.

Uongozi mpya unahitajika kukabiliana na mizozo ya ajira duniani. inasema ILO

Juan Somavia, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Haki za Wafanyakazi (ILO) alipohutubia kikao cha ufunguzi wa Mkutano Mkuu juu ya Masuala ya Mizozo ya Ajira Duniani, uliofanyika Geneva, amependekeza kuwepo “uongozi mpya katika viwango vyote vya kiuchumi na kijamii" ili kusuluhisha vyema mizozo ya ajira kimataifa. Mkuu huyo wa ILO, alisema ulimwengu hauwezi tena kusubiri uchumi ukuwe, kwanza, kwa miaka kadha kabla ya kuamua kuzalisha ajira.

Mkuu wa WHO ahimiza haki kwenye sera za kimataifa

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dktr Margaret Chan aliwaambia wajumbe wa kimataifa, waliohudhuria warsha maalumu uliofanyika Makao Makuu ya UM, kuwacha ile tabia ya “kuamini, bila kuelewa, madai yanayojigamba ustawi wa uchumi na natija zake kimataifa ndio mambo yatakayofanikiwa kumaliza na kuponya matatizo yote ya maisha duniani.”