Afrika

Wataalamu wa UN waitaka Sudan kuacha kutumia nguvu kubwa kuzuia maandamano ya amani.

Hii leo mjini Geneva, Uswisi, wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameeleza hofu yao kuhusu kuongezeka kwa vurugu na kuuawa kwa waandamanaji nchini Sudan ambao wamekuwa wakipinga ongezeko la bei ya bidhaa na uhaba wa mafuta na chakula. Arnold Kayanda na maelezo zaidi.

Ujumuishaji wakimbizi wanufaisha wakimbizi na Rwanda yenyewe

Mpango wa kujumuisha wakimbizi katika maendeleo ya kiuchumi kwenye mji mkuu wa Rwanda, Kigali, umechangia katika wakimbizi kuanzisha biashara ndogo ndogo ambazo zimebuni ajira kwa watu 2,600 nchini humo, ikiwemo biashara ya kuuza mitungi ya gesi inayomilikiwa na mkimbizi kutoka Burundi.

Mwaka 2018 ulikuwa mbaya kwa watoto wanaoishi maeneo ya mizozo- UNICEF

Mwaka 2018 ukifikia  ukingoni, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetoa tathmini ya hali ya watoto mwaka huu hususan kwenye nchi zenye mizozo na kusema ilikuwa ni mbaya kiasi cha kuweka mashakani mustakabali wao.

Ndoto zangu kupinga matumizi ya plastiki sio za abunuwasi:Wakibia

Mwaka 2018 unapofikia ukingoni tunarejelea baadhi ya taarifa ambazo tulizitangaza na tunaamini kuwa zilikuwa na umuhimu mkubwa na miongoni mwao ni ile ya mwanaharakati wa mazingira kutoka Kenya James Wakibia.

Bunge kutotekeleza mapendekezo ya ripoti ni jambo la kusikitisha- Profesa Assad

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali nchini Tanzania, CAG Profesa Musa Assad amezungumzia kitendo cha baadhi  ya ripoti zinazoonyesha  ubadhirifu kutoshughulikia ipasavyo na Bunge la nchi hiyo. Taarifa zaidi na Arnold Kayanda.

Zaidi ya watu milioni 1 walifurushwa makwao DRC mwaka 2018

Zaidi ya watu milioni moja wamefurushwa makwao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwa mwaka 2018 pekee kufuatia mzozo unaondelea nchini humo. Miongoni mwao ni Valentin Muhindo ambaye simulizi yake inaletwa kwako na Grace Kaneiya.

 

Duka langu la vitambaa ni chanzo cha ajira pia kwa vijana Somalia- Amino

Harakati za ujenzi wa Somalia zikiendelea, wananchi wakiwemo wanawake wanachangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo kwa kufanya biashara na kulipa kodi badala ya kusubiri misaada. 

Nchini Kenya, kinyesi cha binadamu chatumika kutengeneza mkaa mbadala

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP linasema mkaa unaotengenezwa kwa kutumia kinyesi cha binadamu unadumu mara mbili zaidi ya mkaa wa kawaida na zaidi ya yote kiwango chake cha uchafuzi wa mazingira ni kidogo mno ikilinganishwa na kiwango cha uchafuzi wa hewa cha mkaa unaotokana na miti. 

FAO na AU zaungana kuondokana na  jembe la mkono Afrika

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO kwa kushirikiana na Muungano wa Afrika, AU wameandaa mfumo utakaowezesha kuzindua kilimo cha kutumia zana za kisasa za kilimo barani Afrika ili kuondokana na kilimo cha jembe la mkono na hivyo hatimaye kuongeza tija na kuvutia vijana kwenye sekta hiyo. 

Ardhi imesalia kuwa mkombozi wangu- Mkulima Somalia

Nchini Somalia, harakati za kuhakikisha wananchi wanashiriki kwenye shughuli za kiuchumi na kijamii zinaendelea kuzaa matunda kwa wananchi ambapo ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini  humo, UNSOM inadhihirisha juhudi hizo kupitia mfululizo wa video zinazonesha wananchi wakishiriki harakati mbalimbali.