Afrika

KM analaani vikali mauwaji huko Guinea Bissau

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa matamshi makali kabisa limelaani mauwaji ya rais wa Guinea Bissau Bernardo Vieira na mkuu wake wa majeshi Tagme Na Waie, na kutoa mwito kwa wananchi, viongozi wa kisiasa na majeshi ya nchi hiyo kubaki makini, kujizuia na kudumisha utulivu. Akisoma taarifa ya baraza hilo balozi wa Libya Ibrahim Dabbashi, ambae ni mwenyekiti wa mwezi huu wa baraza hilo amehimiza kwa pande zote nchini humo kutanzua ugomvi wao kupitia mfumo wa taasisi za kidemokrasia na kupinga jaribiyo lolote la kubadilisha serekali kinyume cha katiba.

UM unaeleza kua mzozo wa kifedha utazidisha umaskini

Utafiti mpya wa Umoja Ma mataifa unaeleza kwamba mzozo wa kifedha duniani unaokumba masoko ya fedha ya Marekani na Ulaya utawathiri watu fukara duniani na kuwatumbukiza mamilioni katika umaskini zaidi na kupelekea vifo vya maelfu ya watoto.

Mabadiliko ya hali ya hewa kuweza kuathiri sana uvuvi duniani

Shirika la UM juu ya Chakula na Kilimo limechapisha ripoti hii leo ikionya kwamba ni lazima biashara ya uvuvi na idara za kitaifa za uvuvi zichukuwe hatua zaidi kufahamu na kujitayarisha kutokana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa kwa uvuvi duniani.

Simu za mkono njia muhimu ya mawasiliano kwa mataifa maskini

Sita kati ya kila watu kumi kote duniani wanasimu ya mkono ikiwa ni ishara kwamba simu hizo ndizo teknolojia ya mawasiliano iliyochaguliwa hasa katika mataifa maskini, hiyo ni kufuatana na ripoti mpya ya UM.

Kikao cha 10 cha Baraza la Haki za Binadamu cha funguliwa Geneva

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu Navi Pillay, ameyahimiza tena mataifa ya dunia kuweka kando tofuati zao na kufanya kazi pamoja kuhakikisha matokeo ya ufanisi katika mkutano wa mwezi ujao dhidi ya kutostahamiliana, ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni huko Geneva.

Hapa na pale

Kikosi cha pamoja cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika na UM huko Darfur kiliripoti Alhamisi kwamba utulivu wa kiasi fulani umerudi katika eneo lililokua na ghasia la Magharibi ya Sudan, ingawa kungali na wasi wasi juu ya kuendelea ghasia katika baadhi za sehemu. UNAMID inasema kumekua na ripoti za uhalifu huko Darfur ya Kaskazini na wanamgambo wenye silaha wanaendelea kuwashambulia na kuwabughudhi raia huko Darfur ya Kusini

Ripoti ya UM yataka mageuzi katika kikosi cha polisi Kenya

Karibuni wapendwa wasikilizaji katika makala yetu ya ripoti ya wiki leo tutazungumzia ripoti ya mjumbe maalum wa UM kwa ajili ya mauwaji ya kiholela, inayo toa mwito kwa Rais wa Kenya kutambua na kuchukua hatua za kukomesha kile alichokieleza ni "mauwaji yanayopangwa, yaliyoenea na kufanywa kwa ustadi" na polisi wa nchi hiyo.

Wasi wasi wa ghasia mpya mashariki mwa JKK

Idara ya huduma za dharura ya UM, OCHA imeeleza wasi wasi wakutokea ghasia mpya dhidi ya wafanyakazi wa huduma za dharura huko jimbo la Kivu ya Kaskazini nchini JKK.

Mahakama maalumu ya Sierra Leone yawapata na hatia viongozi watatu wa waasi

Watu watatu walokiongoza kundi la kikatili la waasi wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sierra Leone wamepatikana na hatia ya uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu na mahakama maalum inayoungwa mkono na UM huko Freetown.