Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeanzisha mashine za kusambaza maji kwa mfumo wa ATM katika masoko yaliyoko katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab. Kuanzishwa kwa vibanda vya maji ni sehemu ya Mpango wa Ujumuishaji wa Kijamii na Kiuchumi wa Garissa, GISEDP, unaoruhusu wakimbizi na jamii wenyeji kushirikiana katika mipango ya maendeleo endelevu.