Afrika

Baraza Kuu lakutana kumuenzi Hayati Magufuli 

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na kikao rasmi cha kumuenzi na kumkumbuka Rais wa 5 wa Tanzania Dkt. John Magufuli aliyefariki dunia tarehe 17 mwezi uliopita.  

IOM na EU wasaidia maelfu ya familia zilizoathiriwa na Nzige wa Jangwani nchini Ethiopia:IOM

“Wakati nzige wa jangwani walipovamia eneo letu kwa ghafla, tulikerwa sana,” anaeleza Galmo Kiyo Waariyo, mkulima anayeishi katika kijiji cha Lafto nchini Ethiopia. “makundi ya nzige yalikuwa makubwa kiasi kwamba yalikuwa yakifunika anga na kuleta giza polepole na muda si muda wananza kutembea kila sehemu.” 

Uhaba wa kimataifa wa ubunifu wa dawa za viauvijasumu wachochea kusambaa kwa usugu wa dawa:WHO

Ulimwengu bado unashindwa kutengeneza matibabu mapya ya kupambana na viuatilifu ya ambayo yanahitajika sana, licha ya kuongezeka kwa tishio kubwa na la haraka la usugu wa za vijiuvijasumu au antibiotics, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, iliyotolewa leo . 

Hojaji ya mtumiaji Habari za UN 2021

Karibu kwenye Hojaji ya mtumiaji wa Habari za UNAsante kwa kukubali kushiriki ili tuweze kuboresha vipindi vyetu viweze kukidhi mahitaji yako. Tafadhali fahamu kwamba majibu hayatosema yametumwa na nani na haitokuchukua zaidi ya dakika 4 kumaliza.

WHO yazindua mpango mpya wa kukabili ugonjwa wa Kisukari

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO limezindua mpango mpya wa kusongesha harakati za kukabiliana na ugonjwa wa kisukari ikiwemo kusaka tiba kwa wale wote wanaohitaji, ikiwa ni miaka 100 tangu kugunduliwa kwa Insulin.

COVAX yawasilisha dozi zaidi ya 350,00 za chanjo ya COVID-19 Niger

Serikali ya Niger leo imepokea Zaidi ya dozi 350,000 za chanjo dhidi ya corona au COVID-19 kupitia mkakati wa kimataifa wa kuhakikisha kila nchi inapata chanjo unaosimamiwa na Umoja wa Mataifa COVAX.

Comoro imepokea dozi 12,000 za chanjo ya COVID-19 kupitia COVAX 

Serikali ya visiwa vya Comoro Jumatatu imepokea dozi 12 za chanjo ya Ccorona au COVID-19 aina ya AstraZeneca kupitia mkakati wa Umoja wa Mataifa wa usambazaji wa chanjo COVAX. 

Wataalam wa UN waishutumu Tanzania na Burundi

Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo Aprili 13, 2021, mjini Geneva Uswisi wamezitaka serikali za Tanzania na Burundi kuheshimu haki za wakimbizi na waomba hifadhi ambao wamekimbia Burundi. 

Wakimbizi 34 wafa maji bahari ya Sham- IOM

Watu 34 wamekufa maji baada ya boti walimokuwa wakisafiria kukimbia machafuko nchini Yemen kuzama kwenye bahari ya Sham ikiwa njiani kuelekea Djibouti.
 

Tunahitaji kubadili mwelekeo ili kujikwamua na athari za COVID-19

Mabadiliko ya mwelekeo yanayolinganisha sekta binafsi na malengo ya kimataifa yahahitajika ili kushughulikia changamoto za siku za usoni, pamoja na zile zilizosababishwa na janga la corona au COVID-19, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hii leo Jumatatu, akihutubia kongamano la Ufadhili kwa ajili ya Maendeleo (FfD).