Afrika

Wazuieni nzige sasa au mbebe gharama kubwa ya kusaidia mamilioni Afrika Mashariki baadaye:WFP/FAO

Itakuwa gharama ndogo kwa sasa kulisaidia shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO   kupambana na nzige Afrika Mashariki  kuliko kuwasaidia mamilioni ya watu katika ukanda huo baada ya mazao yao yote kusambaratishwa, ameonya mkurugenzi mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP David Beasley.

Wanawake 10 watengeneza filamu toka Afrika kupata mafunzo kwa msaada wa UNESCO

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO Audrey Azoulay na mtayarishashi filamu mashuhuri kutoka Japan NaomiKawase leo Alhamisi wametangaza majina 10 ya washindi wa tuzo ya UNESCO kwa ajili ya watayarishaji vijana wa filamu ambao ni wanawake toka barani afrika ilijulikanayo kama Nara Residency for Young African Female Filmmakers.

Wakimbizi zaidi wa Cameroon wamekimbilia Nigeria

Takribani wakimbizi 8,000 kutoka Cameroon wamekimbilia katika majimbo ya mashariki na kaskazini mwa Nigeria katika eneo la Taraba na Cross River katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, imeeleza taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Umoja wa Mataifa wahofia kinachoweza kutokea kutokana na ndege zake kuzuiliwa Libya

Umoja wa Mataifa nchini Libya umesema unasikitika kwamba ndege zake ambazo zinasafirisha maafisa wake kuingia na kutoka Libya, hazijaruhusiwa kutua nchini Libya na jeshi lililojitangaza lenyewe la Libyan National Army, LNA linaloongozwa na kamanda Khalifa Haftar.

watoto wa chini ya miaka 18 ni asilimia 50 ya watu wanaoishi kwenye nchi zenye mizozo:UN

Ingawa watoto hawana jukumu kubwa katika vita, mamilioni miongoni mwao wanajikuta katikati ya machafuko ambayo sio watazamaji bali walengwa, umesema Umoja wa Mataifa ukizinfdua muongozo wa kuwalinda watoto katika hali za vita.

IFAD yatoa ombi la msaada kwa ajili ya kuimarisha maisha ya watu vijijini

Mfuko wa maendeleo ya kilimo duniani, IFAD unatoa wito kwa nchi wanachama kusaidi kuimarisha juhudi zake maradufu kwa ajili ya maisha ya watu wa jamii zilizotengwa kufikia mwaka 2030.

Jamhuri ya Kongo yaongeza chanjo ya polio katika maeneo ya mpaka wake na Cameroon na CAR

Shirika la afya ulimwenguni WHO limesema hii leo wataalamu wa chanjo wameanza kuzunguka katika vijiji vya Sangha maeneo ya kaskazini mwa Jamhuri ya Congo wakitoa chanjo dhidi ya polio inayoweza kuenezwa kutoka katika nchi za jirani.

Vifo vya corona vyazidi 1000, WHO yaitisha jukwaa la utafiti na ubunifu

Shirika la afya duniani WHO linaendesha jukwaa la utafiti na ubunifu ili kuchukua hatua za kimataifa kushughulikia ,mlipuko wa virusi vya corona yaani COVID-2019 ambapo hadi sasa watu 42,000 wameambukizwa na tayari vifo vimefikia zaidi ya 1000.

Watu 120,000 wameathirika na mafuriko Madagascar:UNICEF

Mvua kubwa zilizonyesha kwa wiki mbili zilizopita nchini Madagascar zimeathiri watu 120,000 ikiwakata kabisa na huduma za barabara, kusambaratisha shule 174, na kuwalazimisha watu 16,000 kusalia bila makazi.

Nzige waliovamia Pembe ya afrika hawahitaji visa wala kupitia uhamiaji wanashambulia tu:Lowcok

Janga la nzige limeendelea kuliathiri eneo la Pembe ya Afrika hasa Ethipia, Kenya na Somalia , lakini sasa wameripotiwa pia kubisha hodi Uganda n anchi za Sudan Kusini na Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizo katika tahadhari, kwa mujibu wa mratibu wa Umoja wa Mataifa wa misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA.