Serikali ya visiwa vya Comoro Jumatatu imepokea dozi 12 za chanjo ya Ccorona au COVID-19 aina yaAstraZeneca kupitia mkakati wa Umoja wa Mataifa wa usambazaji wa chanjo COVAX.
Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo Aprili 13, 2021, mjini Geneva Uswisi wamezitaka serikali za Tanzania na Burundi kuheshimu haki za wakimbizi na waomba hifadhi ambao wamekimbia Burundi.
Watu 34 wamekufa maji baada ya boti walimokuwa wakisafiria kukimbia machafuko nchini Yemen kuzama kwenye bahari ya Sham ikiwa njiani kuelekea Djibouti.
Mabadiliko ya mwelekeo yanayolinganisha sekta binafsi na malengo ya kimataifa yahahitajika ili kushughulikia changamoto za siku za usoni, pamoja na zile zilizosababishwa na janga la corona au COVID-19, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa hii leo Jumatatu, akihutubia kongamano la Ufadhili kwa ajili ya Maendeleo (FfD).
Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika, Muungano wa Ulaya EU na Mamlaka ya pamoja ya kiserikali kuhusu maendeleo, IGAD, kupitia mkutano waliofanya kwa njia ya mtandao, wametoa tamko la pamoja kutokana na wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya Somalia.
Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, leo limeonya kuwa uhaba mkubwa wa chanjo dhidi ya COVID-19 utasababisha nchi nyingine zishindew kuanza kampeni za chanjo dhidi ya ugonjwa huo hatari.
Kufuatia hivi karibuni serikali ya Kenya kutangaza nia ya kuzifunga kambi za wakimbizi za Kakuma na Dadaab zinazowahifadhi wakimbizi na wasaka hifadhi takribani 430,000, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNCHR, kupitia taarifa iliyotolewa hii leo mjini Geneva Uswisi, limetangaza kushirikiana na Kenya na kuweka mapendekezo ya hatua za kuchukua ili kupata suluhisho kwa wakimbizi wanaoishi katika kambi hizo.
Ofisi ya kamishna wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa, OHCHR, imeshtushwa na ripoti za hivi karibuni za kuibuka kwa mapigano kati ya makabila ya Masalit na waarabu huko El Geneina jimboni Darfur Magharibi nchini Sudan.
Wanawake wakimbizi waliokumbwa na ghasia na ukatili wanapitia kipindi kigumu siyo tu kimwili bali pia kiakili kutokana na yale ambayo wameshuhudia na kupitia. Ingawa hivyo harakati za Umoja wa Mataifa kupitia wadau wake kama Spotlight initiative zimeanza kuleta tabasamu kwa waathirika hao.
Kamati ndogo ya kamati ya kimataifa ya kushauri shirika la afya la Umoja wa Mataifa ulimwenguni, WHO, kuhusu usalama wa chanjo imesema uhusiano wa binadam kuvia damu baada ya kupatiwa chanjo ya AstraZeneca unawezekana kuwepo lakini bado kuthibitishwa.