Hali ya haki za binadamu nchini Mali inatia wasiwasi wakati huu ambapo usalama na hali ya kibinadamu katika maeneno ya kati na kaskazini mwa nchi hiyo ikiendelea kudorora, amesema mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Mali, Alioune Tine.