Afrika

Ingawa mgogoro umeepukwa mizizi ya kutokuwa na uhakika wa chakula Malawi lazima ikatwe:OCHA

Baada ya ziara ya siku mbili nchini Malawi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA, Mark Lowcok amesema leo Jumamosi kwamba mgogoro wa chakula nchini humo umeepukwa asante kwa misaada ya kibinadamu iliyotolewa na mvua kubwa iliyonyesha, lakini metoa wito wa hatua madhubuti kuchukuliwa ili kushughulikia miziz ya kutokuwepo kwa uhakika wa chakula inayoathiri mara kwa mara taifa hilo.

Nalaani vikali shambulio la kigaidi Moghadishu:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea Alhamisi mjini Moghadishu nchini Somalia na kukatili maisha ya watu wengi.

Elimu habarishi na burudishi imeokoa watoto dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini Ukraine

Hii leo ikiwa ni miaka 20 tangu kuanza kutumika kwa mkataba wa kimataifa dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini na vilipukaji, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetaka hatua zaidi dhidi ya silaha hizo ambazo imesema hazina macho.

OCHA yawaenzi wahudumu wa misaada waliouawa Borno mwaka jana.

Leo ni mwaka mmoja  kamili tangu shambulizi ya kusitikisha kukatili maisha ya wahudumu watatu wa misaada ya kibinadamu kwenye mji wa Rann jimbo la Borno nchini Nigeria.

Surua bado ni tishio kubwa dhidi ya mstakabali wa watoto kote duniani -UNICEF.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeonya kuwa  visa vya ugonjwa wa surua vinaongezeka kwa kiwango kikubwa duniani nchi 10 zikiongoza kwa zaidi ya asilimia 74 ya jumla ya ongezeko na pia nchi nyingine zikiwa zile ambazo awali zilikuwa zimeshatangazwa kuutokomeza kabisa ugonjwa huo.