Afrika

Hebu tuache tabia ya ‘Chukua, Tengeneza, Tumia na Tupa,” asema Bi. Amina J. Mohammed

Mkutano wa nne wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa ukiendelea huko Nairobi, Kenya, Naibu  Katibu Mkuu wa umoja huo Amina J. Mohammed ametaka mwaka huu wa 2019 uwe mwaka wa kuibuka na suluhu zenye mabadiliko dhidi ya uharibifu wa mazingira.

Tusikubali kampuni za sigara zifadhili matukio ya michezo- WHO

Shirika la afya ulimwenguni, WHO linasihi serikali kote duniani kusimamia kwa kina sheria inayozuia kampuni za sigara kufadhili au kutangaza sigara kwenye matukio ya michezo yakiwemo yale ya mbio za magari na pikipiki.

Uharibifu wa mazingira unahatarisha afya za binadamu-UNEP

Uharibifu wa sayari dunia ni mkubwa sana na afya za wakazi wa dunia hiyo zipo hatarini iwapo hatua hazitachukuliwa hivi sasa, imesema ripoti ya hali ya mazingira iliyotolewa hii leo na shrika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP.

Ubunifu pekee ndio utakaotufikisha katika mtakabali tunaoutaka:UNEA

Kwa kutumia ubunifu pekee ndio daraja la kizazi hiki kuweza kuipeleka dunia karibu na mtazamo ulioainishwa kwenye  mustakabali tunaoutaka kwa ajili ya wote ifikapo mwaka 2030. 

Maafisa wenye mamlaka wamehusika na ukiukwaji wa haki Sudan Kusini - Ripoti

Ripoti ya tume ya  Haki za Binadamu nchini Sudan Kusini  iliyowasilishwa leo mijini Geneva Uswisi, imebaini kuwa watu 23 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita waliokuwa katika ngazi ya mamlaka nchini humo, wanakabiliwa na tuhuma za ukiukwaji  mkubwa wa haki za binadamu chini ya sheria za kimataifa kwa kutekeleza uhalifu mkubwa unaohusiana na vita nchini Sudan kusini.

Taswira ya wanawake viongozi duniani licha ya hatua haijafikia 50-50-UN

Mkutano wa 63 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW, ukiwa umeingia siku ya pili kwenye mako makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, hii leo baadhi ya mada ambazo zimejadiliwa ni wanawake na uongozi.

Zaidi ya nusu ya watu wote duniani wanakosa huduma ya afya-ILO

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la kazi ulimwenguni iliyotolewa hii leo mjini Geneva Uswisi, zaidi ya nusu ya idadi ya watu wote duniani wanakosa huduma ya afya na ni asilimia 29 tu ambao wanapata huduma kwa mfumo wa bima ya afya.

UNHCR yahitaji fedha zaidi kusaidia wakimbizi wa ndani Burkina Faso

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linahitaji fedha za nyongeza kwa ajili ya kufanikisha operesheni zake za kusaidia wakimbizi wa ndani nchini Burkina Faso wakati huu ambapo dola milioni 27.3 zilizoombwa kwa ajili ya operesheni za mwaka 2018 zimefadhiliwa kwa asilimia 26 pekee.

Mafuriko yasababisha maafa Malawi, Katibu Mkuu UN atuma salamu.

Kwa mara nyingine Malawi imekumwa na mafuriko makubwa yaliyokatili maisha ya watu, kusababisha uharibifu mkubwa na kuwafungisha virago mamia ya watu ambao sasa wanahitaji msaada umesema Umoja wa Mataifa.

CSW63 kuanza leo New York, Marekani, mustakabali wa wanawake na wasichana kuangaziwa

Mkutano wa 63 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW unaanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ukileta pamoja zaidi ya washiriki 9000 kutoka wawakilishi wa nchi 193 wanachama wa umoja huo pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa na yale ya kiraia.