Habari Mpya

Serikali ya mpito Sudan Kusini yaundwa, Guterres apongeza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekaribisha hatua ya kuundwa kwa serikali ya mpito ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, TGoNU, hii leo.

WHO yaeleza hofu yake kubwa zaidi juu ya virusi vya Corona

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limesema kuwa hofu yake kubwa zaidi hivi sasa ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Corona, COVID-19 kuingia katika mataifa yenye mifumo dhaifu ya afya hususan barani Afrika.

Janga lililosababishwa na binadamu Syria likome sasa- Guterres

“Hakuna suluhu ya kijeshi kwenye mzozo wa Syria,”  amesisitiza tena hii leo Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa António Guterres huku akitoa wito kwa kumalizwa kwa janga hilo lililosababishwa na binadamu na kuleta machungu ya muda mrefu kwa wananchi wa Syria.

WHO yaingiwa hofu na mwenendo wa maambukizi ya virusi vya Corona, COVID-19

Shirika la afya ulimwenguni, WHO, limesema hofya yake hivi sasa juu ya kuenea kwa virusi vya Corona, COVID-19 ni kutokuwa na taarifa za wazi kuhusu uhusiano wa kuenea kwa virusi hivyo, kama vile historia ya mtu kusafiri China au kuwa na mawasiliano na mtu aliyethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.

Kulikoni harakati za kutokomeza ukoloni zimedorora?

Maeneo 17 duniani bado yanatawaliwa na harakati za kusaidia maeneo hayo zinaonekana kudorora, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo jijini New York, Marekani wakati akifungua mkutano wa mwaka huu wa 2020 wa kamati maalum kuhusu kutokomeza ukoloni duniani.

Cameroon wajibika katika ulinzi wa raia wanaokumbwa na ukatili- UN

 

Umoja wa Mataifa kupitia maafisa wake waandamizi umetoa wito wa kuchukua hatua zaidi ili kulinda raia wanaokabiliwa na ghasia huko nchini Cameroon.

Athari za kiuchumi za virusi vya corona huenda zikasikika hadi nje ya China-IMF

Wakati idadi ya maambukizi ya virusi vya corona COVID-19 ikiendelea kuongezeka kila uchao, Shirika la afya ulimwenguni, WHO limehimiza jamii ya kimataifa kuwekeza katika suluhu za afya ambazo zinaweza kusaidia katika kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo sasa na wakati huo huo kusaidia katika kujiandaa kwa ajili ya kuwekeza katika jamii kwa siku za usoni.

Watu zaidi ya 700,000 watawanywa na machafuko Sahel:UNHCR

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na washirika wake wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya wakimbizi na wakimbizi wa ndani katika eneo la Sahel huku mashambulizi dhidi ya raia yakiongezeka.

Lugha ya Kiswahili yazidi kupaa duniani-UNESCO

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya lugha mama, Umoja wa  Mataifa umepigia chepuo lugha ya Kiswahili ikisema kuwa ni miongoni mwa lugha inayozidi kupanuka kimatumizi duniani na kusaidia kueneza utamaduni wake.

Kwa heri Kakuma! Narejea Ethiopia lakini katu sitosahau Kenya- Mkimbizi

Kundi la wakimbizi 76 kutoka Ethiopia waliokuwa wanaishi kwenye kambi  ya Kakuma nchini Kenya wamerejea nyumbani ikiwa ni mara ya kwanza ya  utekelezaji wa mpango wa kurejea nyumbani kwa hiari kwa wakimbizi hao wa Ethiopia.