Habari Mpya

Mkuu wa haki za binadamu amelaani mauaji ya raia Ivory Coast

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameelezea hofu juu ya kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Ivory Coast. Amesema mashambulizi dhidi ya raia hayakubaliki na kulaani mauaji ya jana kwenye kitongoji cha Abobo mjini Abidjan ambako makombora yamekatili maisha ya watu takriban 30 na kujeruhi wengine wengi.

Hakuna haja ya kuzuia watu kwenda Japan:WHO/WMO

Hakuna mipango ya mara moja ya kuweka vikwazo vya usafiri kuingia na kutoka Japan yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Wahamiaji zaidi ya 50,000 wahamishwa Libya na IOM/UNHCR

Operesheni ya pamoja ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM imesaidia kuwahamisha maelfu ya wahamiaji kutoka nchini Libya.

Libya yasema itatekeleza azimio la baraza la usalama 1973

Baada ya azimio la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa namba 1973 lililopitishwa jana usiku likimtaka kanali Muammar Qadhafi kutekeleza mara moja usitishaji wa mapigano na likimuwekea vikwazo vya safari za anga kuzuia utawala wake kutumia nguvu za anga dhidi ya watu wa Libya, leo serikali ya Libya imetangaza kusitisha mapigano mara moja na operesheni zote za kijeshi.

Baraza la usalama la UM limeiwekea Libya vikwazo vya safari za anga

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuiwekea vikwazi vya anga Libya ili kuzuia majeshi ya anga ya nchi hiyo kushambulia raia.

Afghanistan itaendelea kuhitaji msaada wa kimataifa

Afghanistan inahitaji msaada wa kimataifa unaoendelea kama kweli inataka kuchukua majukumu ya nchi hiyo Machi 21 amesema balozi wa Afghanistan kwenye Umoja wa Mataifa Zahir Tanin.

Mtangazaji wa Canada awa balozi wa WFP dhidi ya njaa

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mpango wa chakula WFP imemwidhinisha mtangazaji wa zamani kutoka Canada George Stroumboulopoulos kuwa balozi wake wa masuala ya njaa.

Ban ahitimisha ziara Guatemala na anaelekea Afrika Kaskazini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amejadili na viongozi wa amerika ya Kati kuhusu hali inayoendelea katika ulimwengu wa Kiarabu na Afrika ya Kaskazini hususan Libya.

Mjadala kuhusu haki ya ardhi kwa watu wa asili ni muhimu:UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili James Anaya ametoa wito wa mawasiliano zaidi baina ya serikali, watu wa asili na makabila huko Surinam na kuahidi kuendelea kusaidia juhudi za haki za watu hao za kumiliki ardhi na rasilimali zingine.

Maambukizi ya HIV kutoka kwa mama hadi kwa mtoto kudhibitiwa

Wadau muhimu wanaojihusisha na masuala ya HIV na ukimwi wamekubaliana njia muafaka ya kusaidia kutokomeza maambukizi ya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto Mashariki na Kusini mwa Afrika.