Habari Mpya

Hali nchini Syria bado ni tete, huku maandamano yakiendelea

Jumla ya watu sita wameripotiwa kuuawa na maafisa wa usalama siku ya Ijumaa kwenye mji ulio kusini mwa Syria Daraa baada ya maelfu ya watu kuingia mitaani kuandamana wakitaka kuwe na uhuru wa kisiasa na kumalizika kwa ufisadi.

Uvumbuzi wahitajika kukidhi mahitaji ya maji mijini:FAO

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO linasema kuwa kunahitajika kufanyika uvumbuzi mpya ili kuhakikisha kuwa kuna maji ya kutosha na salama kwa wanaoishi mijini kwenye nchi zinazoendelea wakati kunapoendelea kushuhudiwa kuongezeka kwa watu kwenye sehemu za miji.

Hali yazidi kuwa mbaya nchini Bahrain:UM

Huku hali ikiendelea kuwa mbaya nchini Bahrain watu zaidi wanaripotiwa kutoweka huku kati ya watu 50 na 100 wakiwa hawajulikani waliko kwa muda wa wiki moja iliyopita.

Hatua zahitajika kusaidia hali ya kibinadamu Lampedusa:

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linatoa wito kwa serikali ya Italia kusaidia kupunguza msongamano ulio katika kisiwa cha Lampedusa.

Maelfu ya Walibya wakimbia makwao wakitawanyishwa na machafuko:UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa wanaoikimbia Libya na kuvuka mpaka wanasema maelfu ya watu wamekimbia makwao mashariki mwa nchi na kuchukua hifadhi kwenye mashule na kumbi za vyuo.

Mikakati ya kudhibiti mihadarati ifikiriwe upya:UNODC

Afisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa nchi kufikiria upya mikakati ya kimataifa ya udhibiti wa madawa huku kukiwa na changamoto ya madawa hayo kuwa tishio kwa afya ya jamii, usalama na maendeleo.

Baada ya duru ya pili ya uchaguzi Haiti yasubiri matokeo

Hamasa inaongezeka nchini Haiti wakati mamilioni ya watu wakisubiri matokeo ya uchaguzi wa Rais wa duru ya pili uliofanyika jana Jumapili.

Makubaliano ya Brazili na Marekani yaifurahisha ILO

Mkurugenzi wa shirika la kazi duniani ILO Juan Somavia ameyakaribisha maelewano yaliyo tiwa sahihi kati ya serikali ya Marekani na Brazil yaliyo na lengo la kutatua tatizo la ukosefu wa ajira na masuala mengine ya kijamii kati ya mataifa hayo.

Chanjo dhidi ya polio yaanza nchini Somalia

Maafisa wa afya nchini Somalia wameanzisha kampeni ya siku tatu inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ya kuwachanja zaidi ya watoto milioni 1.8 dhidi ya ugonjwa wa Polio miaka minne baada ya taifa hilo kutangazwa kutokuwa na ugonjwa huo.

Wahamiaji zaidi wawasili Lampedusa Italia:IOM

Kuwasili kwa wahamiaji zaidi ya 1630 kwenye kisiwa cha Lampedusa Italia jana Jumapili na usiku wa kuamkia leo kumesababisha mrundikano mkubwa kwenye kituo cha wahamiaji ambapo IOM na washirika wake wanatoa msaada wa mapokesi na ushauri wa kisheria kwa wahamiaji, waomba hifadhi na watoto wasioambatana na mtu yeyote.