Habari Mpya

Mabadiliko Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini yatatoka ndani ya eneo hilo asema Ban na kuwa UM uko tayari kusaidia

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa limekutana leo mjini New York kutathimini na kupitisha mswada wa azimio la baraza la haki za binadamu la kuisitisha uanachama Libya.

Tusiwasahau na wengine wanaokumbwa na machafuko:IOM

Shirika la Umoja wa mataifa la uhamiaji IOM limeonyesha wasiwasi kutokana na kuendelea kuongezeka kwa wakimbizi wa ndani nchini Ivory Coast ambayo imetumbukia kwenye mkwamo wa kisiasa tangu duru ya pili ya uchaguzi wa rais mwaka jana.

Zimbabwe imetakiwa kuwaachilia wanaharakati waliokamatwa

Serikali ya Zimbabwe imetakiwa kuwaachilia kundi la wanaharakati wa kijamii walioshitakiwa kwa uhaini baada ya kujadili matukio yanayoendelea Misri na Libya.

Mkuu wa UNICEF azuru DRC kutathimini hali ya watoto

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Athony Lake amewasili mjini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hii leo ili kukutana na maafisa wa serikali na kuzuru maeneo ambayo maafisa wa afya wanakabiliana na mlipuko unaosambaa haraka wa polio.

LRA waendelea kushambulia Mashariki mwa DRC:UNHCR

Ghasia na mashambulizi dhidi ya raia yanayofanywa na kundi la Lords Resistance Army (LRA) la Uganda Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ymaeendelea kuongeza hofu kwa mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR.

Wafuasi wa Ouattara wamekwama Abijan:UNHCR/UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linaendelea kutiwa hofu na hali ya raia ambao ni wafuasi wa Alassane Ouattara nchini Ivory Coast ambao wamekwamba kwenye wilaya ya Abobo mjini Abijan kufuatia mapigano ya hivi karibuni.

Mkuu wa haki za binadamu aionya serikali ya Yemen

Kamishina mkuu wa wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameionya serikali ya Yemen kwa ghasia na ukandamizaji dhidi ya wanaofanya maandamano ya amani nchini humo na ameitaka serikali kulinda haki za waandamanaji na waandishi wa habari chini ya sheria za kimataifa.

Hali yazidi kuwa mbaya kwenye mpaka wa Tunisia na Libya

Hali imeelezewa kuzidi kuwa mbaya kwenye mpaka baina ya Libya na Tunisia huku idadi ya watu ikiongezeka.

Wahisani wakutana Geneva kuomba fedha kuisaidia Libya

Mashirika ya kimataifa ya misaada yanaongeza juhudi kuwasadia maelfu ya wafanyakazi wahamiaji waliokwama kwenye mpaka wa baina ya Libya, Misri na Tunisia.