Habari Mpya

Watoto wa mitaani wasiwe adha bali wasaidiwe:Pillay

Idadi ya watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani duniani sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 100 kwa mujibu wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

UNHCR na IOM yataka msaada zaidi kwa wanaokimbia Libya

Wakihitimisha ziara ya siku mbili nchini Tunisia mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na yule wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM wametoa wito wa kuendelea kwa juhudi za kimataifa kuwasaidia maelfu ya watu wanaokimbia machafuko Libya.

Pande zinazopigana Afghanistan lazima zihakikishe zinawalinda raia:Ripoti ya UM

Pande zinazopigana nchini Afghanistan lazima ziongeze juhudi za kuwalinda raia mwaka huu 2011 umesema mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA na tume huru ya haki za binadamu nchini Afghanistan katika ripoti yao ya mwaka 2010 ya ulinzi wa raia katika maeneo ya vita.

Wakenya Sita wametakiwa kufika mahakama ya ICC

Wakenya sita wanaoshukiwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya uliozua utata 2007 wametakiwa kufika mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC mjini The Hague tarehe 07 April.

Mahojiano na Dr wa UNAMID kuhusu siku ya wanawake duniani

Wakati dunia leo ikiadhimisha siku ya kimataifa ya wanawake na miaka 100 tangu kuanza kuadhimishwa siku hiyo, ofisi mbalimbali za Umoja wa Mataifa zinazoendesha operesheni katika nchi mbalimbali zimekuwa msitari wa mbele katika juhudi za ukombozi wa mwanamke.

Njia bora za kilimo zinaweza kuongeza uzalishaji: De Schutter

Wakulima wadogowadogo wanaweza kuongeza mara mbili uzalishaji wa chakula katika kipindi cha miaka 10 endapo watatumia mifumo ya ikolojia katika maeneo ambayo yanakabiliwa na njaa.

Wanawake milioni 16 wanaishi na virusi vya HIV:UNAIDS

Kati ya watu milioni 34 wanaoishi na virusi vya HIV milioni 16 kati yao ni wanawake na idadi inaongezeka kwa mujibu wa Mariangela Simao mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na ukimwi UNAIDS.

Nchi zaidi zimetia sahihi mkataba kulinda bayo-anuai

Colombia, Denmark, Netherlands na Sweden zimekuwa nchi za kwanza kutia sahihi mkataba mpya kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ulio na sheria za kimataifa kuhusu hatua zitakazochukuliwa iwapo kutaokea uharibifu kwenye balojia anuai na viumbe unaosababishwa na viumbe vilivyofanyiwa mabadiliko ya kimaumbile.

Ushahidi unaopatikana kwa njia ya mateso upuuzwe:UM

Mtaamu huru wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya mateso ametaka ushahidi unaopatikana baada ya kufanyika vitendo vya kuwatesa watuhumiwa usipewe uzito wowote tena.

Wasichana vigori wana mchango mkubwa:UNICEF

Ikiadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo imeenda sambamba na kutimia kwa maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanza kuazimishwa kwa siku hii,shirika la umoja wa mataifa linalohusika na watoto UNIECEF limesema kwamba wasichana vigori wanamsaada mkubwa kwa familia zao pamoja na jamii kwa ujumla.