Habari Mpya

IOM yafungua zahanati mpaka wa Kenya na Uganda

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na baraza la kupambana na Ukimwi nchini Kenya wamefungua zahanati mpya ya kutoa matibabu ya bure ili kuwafikia wasio na uwezo wa kugharamia matibabu na wanaosafiri kati ya mpaka wa Kenya na Uganda.

Watu zaidi waendelea kukimbia machafuko Libya:UM

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa linaendelea kupokea ripoti za watu wanaondelea kuhama makwao mashariki mwa Libya.

Hali yazidi kuwa mbaya Ivory Coast:UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa maelfu ya watu wanaohofia kutokea kwa vita wanaendelea kukimbia makwao kwenye mji mkuu wa Ivory Coast Abidjan na sehemu zingine za magharibi mwa nchi.

Ban Ki-moon atiwa moyo na ari ya vijana Misri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa ametiwa moyo na jinsi vijana nchini Misri wanavyojaribu kujenga demokrasia mpya kwenye taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.

Watu wanpashwa kuelimishwa kuhusu utumwa na biashara ya utumwa:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa biashara ya utumwa ilisababisha mateso makubwa kwa mamilioni ya watu wasio na hatia kwa muda wa karne nne.

Serikali ya Libya inakaidi azimio la baraza la usalama:Ban

Serikali ya Libya haijaacha mashambulizi au kutangaza kusitisha mapigano kama ilivyotakiwa na azimio la baraza la usalama kwa mujibu wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Uingereza na Australia yaipa IOM zaidi ya dola milioni 6 kwa ajili ya kuendelea kusafirisha wahamiaji

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limesema linaendelea na shughuli ya kuwasafirisha maelfu wa wahamiaji wanaokimbia machafuko Libya baada ya kupata msaada wa fedha.

Zaidi ya 460 wafariki dunia Ivory Coast kutokana na mchafuko:UM

Zaidi ya watu 460 wamekufa nchini Ivory Coast tangu mwezi Desemba mwaka jana kufuatia utata uliozuka kwenye uchaguzi mkuu wa Rais katika taifa hilo la Afrika ya Magharibi.

Msaada unahitajika kwa ajili ya Japan:Michael Douglas

Mcheza filamu mashuhuri na mjumbe maalumu wa amani wa Umoja wa Mataifa Michael Douglas amesema dunia inahitaji kuendelea kuisaidia Japan hasa wakati huu.

NGO's kuusaidia UM kupambana na mihadarati

Mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGO\'s yako tayari kuusaidia Umoja wa Mataifa kupambana na tatizo la mihadarati.