Habari Mpya

UNHCR yasifu ufunguaji mipaka kuruhusu wakimbizi wa Libya

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limesema limetiwa moyo na uamuzi wa serikali ya Tunisia na Misri ambazo zimetanagaza kuendelea kuacha wazi mipaka yake ili kuruhusu wakimbizi kutoka nchi jirani ya Libya kupita kwenye maeneo hayo.

ICC yasema wananchi wa Libya ndiyo wanaoweza kuamua hatma ya haki yao

Mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa juu ya uhalifu Luis Moreno-Ocampo, amesema uamuzi wa kuona haki na usawa unatendeka nchini Libya upo mikononi mwa wananchi wenyewe.

Kuna mianya mikubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu Ivory Coast:UM

Ripoti mpya iliyotolewa na kamishna wa umoja wa mataifa juu ya haki za binadamu imeainisha maeneo kadhaa ambayo yanaendelea kukwaza misingi ya haki za binadamu nchini Ivory Coast tangu nchi hiyo ifanye duru ya pili ya uchaguzi wa rais.

Wasomalia 57 wafariki dunia baada ya kuzama kwenye pwani ya Yemen

Kiasi cha watu 57 raia wa Somalia wamerafiki dunia baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama maji katika pwani ya Yemen.

Timor-Leste imeachana na enzi za vita, na kukaribisha maendeleo- Waziri Mkuu

Wananchi wa taifa la Timor-Leste hatimaye wameingia kwenye duru mpya ya mashikamano na maendeleo na kuiaga enzi ya machafuko na mizizo iliyokumba eneo hilo kwa miaka mingi.

Kenya yaanza mikakati kuwakoa watumiaji wa madawa ya kulevya dhidi ya HIV

Serikali ya Kenya imeanza kuchukua hatua za ziada ili kukabiliana na maambukizi

ya virusi vya HIV kwa watumiaji wa madawa ya kulevya.

Kuwekeza kwa wanawake ndiyo suluhu ya ukuzaji uchumi-Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro amesema uwezekaji kwa

wanawake na watoto wa kike, ni jambo muhimu linaloweza kusukma mbele maendeleo

ya nchi na wakati huo huo ni njia mujarabu ya kuwawezesha wanawake.

KM Ban awalaani maharamia wa Somalia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amevunjwa moyo na

kusikitishwa kufuatia ripoti za mauwaji kwa raia wanne wa kimarekani waliotekwa

na maharamia katika pwani ya Somalia.

UM watia ushawishi wake kutanzua mzozo wa Sudan Kusini

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan UNMIS, umekuwa na juhudi za kidiplomasia

ya uletaji suluhu baina ya makundi yanayohasimiani katika eneo la kusini la nchi

hiyo.

Wahamiaji wa Libya wakimbia mapigano

Wahamiaji kutoka Libya wameanza kuvuka mipaka na baadhi yao wameripotiwa kupiga

hodi nchini Tunisia wakijaribu kusaka hifadhi kutokana na machafuko

yanayoendelea katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.