Habari Mpya

Libya inaendesha "mauwaji ya halaiki"

Serikali ya Libya imeshutumiwa kuwa inaendesha mauji ya halaiki na huku ikifanya matukio makubwa ya ufunjifu wa haki za binadamu ikiwemo kuwatesa raia wake na kuwaweka kizuizini.

Mkuu wa ILO ajiunga na wengine kulaani utumiaji nguvu dhidi ya waandamanaji Libya

Kiongozi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi ameongeza sauti yake kwa kulaani viongozi wa Libya kwa mauaji dhidi ya wapinzani na kuashiria kwamba Libya ni mfano tosha wa hatari ya kukosekana ajira na umasikini ndani ya taifa.

Baraza la Usalama laongeza muda wa vikosi vya kulinda amani Timor-Leste

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza alhamisi hii muhula wa kuwepo vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Timor ya Mashariki kwa mwaka mmoja.Tume hii inayojulikana kama UNMIT itafanya kazi hadi tarehe 26 mwezi februari mwaka wa 2012.

KM Ban ataka Hollywood kuipiga jeki tuzo la Oscar kwa UM

Akitumia karata ya tuzo ya Oscar iliyotwaa Umoja wa Mataifa miaka 60 iliyopita kupitia filamu iliyoelezea hali ngumu za watoto wenye ulemavu, Katibu Mkuu Ban Ki-moon ameanza kuishawishi Hollywood ili kukusanya fedha na hatimaye kuisambaza filamu hiyo duniani kote.

Ukosoaji siyo uchochezi: Mjumbe wa UM Cambodia

Mjumbe huyo amesema kuwa kukosoa jambo siyo dhambi wala uchochezi hivyo mamlaka lazima zitambue kwamba wakosoaji wa haki za binadamu wanafanya hivyo kama njia ya kujenga jamii adilifu na yenye kuheshimu misingi ya kibinadamu.

Hali ya usalama Afghanistan bado ni tete:UM

Mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan amesema kuwa hali ya usalama katika nchi hiyo bado ni ya kiwango cha chini ambayo imechochewa na kuondolewa madarakani kwa utawala wa Taliban mwaka 2001.

Kiongozi mkuu wa polisi wa Serbia katika Kosovo apatiwa kifungu cha miake 27

Kiongozi mkuu wa zamani wa polisi wa Serbia amehukumiwa kifungo cha miaka 27 jela kwa kuhusika na uhalifu dhidi ya binaadamu na uhalifu wa kivita dhidi ya raia wa Albania wa Kosovo katika mwaka 1999.

Mwakilishi wa UM Somalia ayapuuza madai ya kiongizi wa Djibouti

Mwakilishi maalumu wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Augustine Mahiga ameyapuzilia mbali madai yaliyotolewa na kiongozi mmoja wa upinzani wa Djibouti aliyetuhumu askari wa Umoja wa Mataifa wanapatiwa mafunzo kwamba walitumia ushawishi kuwakandamiza waandamaji.

UM unamatumaini na machipuo mapya Tunisia

Ripoti iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na haki za binadamu imeilezea Tunisia kama taifa linalochanua upya kutoka kwenye mfumo wa ukandamizaji na kuingia kwenye ukurasa mpya unaozingatia na kuheshimu mifumo ya haki za binadamu.

Afisa wa ngazi ya juu jeshini DRC atupwa jela kutokana na ubakaji

Kiongozi wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Congo, amepongeza na kukaribisha uamuzi wa mahakama moja ambayo imemkuta na hatia afisa wa jeshi juu ya makosa ya ubakaji na ukiukaji wa haki za binadamu.