Habari Mpya

UNAIDS imetaka kuwepo na uhuru wa kimataifa wa kutembea kwa watu wanaishi na virusi vya HIV

Mkuu wa Bodi la Jumuiya ya Mashirika ya UM dhidi ya ukimwi (UNAIDS) Michel Sidibe, ametoa wito wa kuwepo uhuru wa kimataifa wa kutembea kwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kwa mwaka huu wa 2010, mwaka ambao nchi mbalimbali zimeazimia kufikia malengo ya kimataifa ya kuzuia virusi vya ukimwi, kupata matibabu, huduma na msaada unaohitajika kwa wanaoishi na virusi hivyo.

Zimbabwe kufaidika na dola milioni 1.5 ufadhili wa Uholanzi:IOM

Msaada mpya wa dola za Kimarekani milioni 1.5 kutoka serikali ya Uholanzi utasaidia kuchagiza shughuli za kibinadamu za shirika la kimataifa la uhamiaji IOM nchini Zimbabwe kwa kipindi cha mwaka mmoja.

WFP imesitisha msaada Kusini mwa Somalia

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limesema vitisho vya kundi la wanamgambo al Shaabab linalodhibiti asimilia 95 ya eneo la kusini mwa Somalia limeathiri shughuli zake za misaada.

Idadi kubwa ya watoto njiti wanazaliwa Afriks na Asia:Yasema WHO

Kuna tufauti kubwa kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea katika fursa ya kuishi watoto wanaozaliwa kabla ya siku kutimia au njiti.. Takribani watoto njiti milioni 13 wanazaliwa kila mwaka duniani kote, hii ni kwa mujibu kwa takwimu za shirika la afya duniani WHO zilizochapishwa jumatatu.

Eritrea imeishutumu Ethiopia kwa mashambulizi ya kijeshi!!

Eritrea imeishutumu Ethiopia kwa kufanya mashambulizi siku ya jumapili kwenye mpaka wanaozozania, lakini imedai majeshi yake yaliwafurusha na kuwauwa wanajeshi 10 wa Ethipia na kuwakamata wengine wawili.

Mjumbe Maalamu wa Umoja wa Mataifa ameitaka Sudan kujitahidi kupata utulivu na amani mwaka huu wa 2010

Mjumbe maalumu wa umoja wa mataifa nchini Sudan, Ashraf Qazi amewatolea wito watu wote wa Sudan kushikamana kutafuta amani zaidi 2010.

Eide ameonya kuendelea kwa mtafaruku wa kisiasa baada ya bunge la Afghanistan kulikataa Baraza la Mawaziri lililoteuliwa

Kukataliwa na wabunge sehemu kubwa ya baraza hilo jipya la Rais Hamid Karzai ni pigo la kisiasa kwa nchi hiyo, amesema Mjumbe Maalumu wa KM nchini Afghanistan Kai Eide .