Haiti imekumbwa tena na tetemeko kubwa Ijumatano, na kutikisa majengo na kusababisha mtaharuku mkubwa, watu wakikimbia barabarani baada ya kushuhudia mtetemeko mkubwa ulosababisha maafa siku nane zilizopita.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaripoti kwamba wanafanya maendeleo makubwa katika kufikisha msaada wa dharura unaohitajika sana na maelfu ya walonusurika tetemeko la ardhi huko Haiti.
Majadiliano juu ya kupunguza silaha za nukilia duniani hayakuweza kuanza Ijumanne wakati Pakistan ilipozuia kuidhinishwa kwa ratiba ya 2010 ya mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya kupunguza silaha huko Geneva.
Mkurugenzi mkuu wa Idara ya mazingira ya UM Achim Steiner anasema ni lazima kwa majadiliano ya kimataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani yabaki chini ya uwongozi wa UM hata ikiwa mkutano wa viongozi wa Copenhagen mwezi Disemba haukufanikiwa kuleta ufumbuzi.
Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR), iliwapokea watu wepya elfu 77 802 kutoka Pembe ya Afrika mwaka 2009 ikiwa ni muongezeko wa asili mia 55 kulingana na mwaka 2008 na mara ya kwanza wa-Somali hawakua wengi kuliko watu wa mataifa mengine alieleza afisa wa uhusiano wa mambo ya kigeni wa idara hiyo Rocco Nuri.
Kukiwa na idadi kubwa kabisa ya watu walopoteza makazi yao kutokana na tetemeko la ardhi huko Haiti na ukosefu wa vifaa kuweza kutawanya msaada wa dharura, mashirika ya kimataifa na serekali zimeanza mipango ya kujenga makazi makubwa ya muda.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameahidi kuharakisha msaada mkubwa wa huduma za dharura unaohitajika kusaidia wa Haiti walokumbwa na mtetemeko mkubwa wa ardhi wiki iliyopita.
Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu Navi Pillay aliihimiza serekali ya Uganda siku ya Ijumaa kutupilia mbali mswada wa sheria kuhusiana na watu wa jinsia moja wanaopendana, ambao unatarajiwa kufikishwa bungeni mwishoni mwa mwezi Januari.