Habari Mpya

Myanmar yatajwa kama moja ya nchi inayotengezaji mabomu ya ardhini

Taifa la Myanmar limetajwa kuwa taifa tu linelotengeza mabomu ya ardhini. Kulingana na uchunguzi wa kimataifa kuhusu matumizi ya silaha ni kuwa Myanmar ni mmoja ya watengezaji wa mabomu ya ardhini huku watengezaji wengine wakiwa ni India na Pakistan.

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya UM aunga mkono kutekelezwa kwa mkataba ya kutoweka kwa watu

Mkuu wa tume ya Umoja wa Kimataifa ya haki za binadamu Navi Pillay ameunga mkono kuanza kutumika kwa mkataba mpya wa haki za binadamu wa kutokomeza kutoweka kwa lazima na kuwachukulia wahusika hatua na pia kuwalinda waathiriwa.

Mkutano wa nchi za kusini waendelea Geneva

Maonyesho ya kimataifa ya maendeleo kwa sasa yanafanyika mjini Geneva nchini Uswisi ambapo wajumbe zaidi ya 600 kutoka nchi 150 wanahudhuria.

Siku ya kimataifa kutokomezwa kwa dhuluma dhidi ya wanawake kuadhimishwa kesho tarehe 25

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa kuna hatua zilizopigwa kote duniani ambapo watu wanaungana kumaliza dhuluma dhidi ya wanawa na watoto wasichana.

UM wataka kurejewa kwa mazungumzo mashariki ya kati

Umoja wa Mataifa umetaka kuondoshwa kiwingu kinachotatiza kuanza tena mazungumzo ya mashariki ya kati ambayo yalivunjika hivi karibuni kufuatia Israel kuendeleza na ujenzi wa makazi ya walowezi katika ukingo wa Gaza.

MONUSCO yaanza operesheni ya kuwalinda raia na watoaji misaada ya kibinadamu

Vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa vilivyopo Jamhuri ya kidemokrasia (DRC) vimetangaza kuanzisha oparesheni maalum yenye lengo la kuwalinda raia wa nchi hiyo pamoja na wafanyakazi wa kutoa misaada dhidi ya makundi ya waasi ambayo yamekuwa yakichafua hali ya hewa kwenye eneo hilo.

UM umelaani vikali shambulio la Korea Kaskazini:Ban

Shambulio la leo la makombora lililofanywa na Korea ya Kaskazini kwenye kisiwa cha Yeongpyeong Korea Kusini limelaaniwa vikali na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Ban awataka vijana kuunga mkono UM kufikia malengo ya wengi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka vijana kuunga mkono harakati za Umoja huo wa Mataifa, kuhakikisha dunia inaendelea kuwa salama na kimbilio la wengi, pamoja na kwamba changamoto zinazoendelea kuibuka nyakati hizo ni kubwa zisizowahi kushuhudiwa wakati wowote.

Uandikishaji kura ya maoni Kaskazini mwa Sudan hauridhishi:UM

Kumekuwa na mwamko mgodo wa wananchi wa Sudan Kusin ambao wanaishi upande wa pili yaani Sudan Kaskani wanaojitokeza kujiandikisha kwenye daftari la upigaji kura kwa ajili ya kura ya maoni itayofanyika January mwakani.

Mipango miji salama kwa wanawake yazinduliwa Delhi

Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya akina mama limezindua mpango wa kimataifa wa kuifanya miji kuwa salama kwa wanawake mjini New Delhi nchini India wakati wa kuanza kwa mkutano wa kimataifa kuhusu usalama wa wanawake.