Habari Mpya

Mabadiliko kwenye kilimo lazima kupunguza gesi chafu:Cancun

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala ya haki ya kupata chakula ameonya kuwa bila kuwepo kwa hatua madhubuti viwango vya gesi inayochafua mazingira vinavyotokana na kilimo vinatarajiwa kuongezeka kwa asilimia hamsini ifikapo mwaka 2030.

Juhudi imara za amani zatakiwa wakati UM ukiadhimisha siku ya kimataifa ya mshikamano kwa Wapalestina

Kila mwaka siku ya kimataifa ya mshikamano kwa ajili ya watu wa Palestina inatathimnini hali ya Wapalestina na kufikiria nini kifanyike zaidi kuleta amani ya kudumu.

Afrika iko hatarini kupoteza vyanzo vya maji:UNEP

Utafiti mpya ulioangazia hali ya upatikanaji wa maji safi ya kunywa umetaja changamoto zinazozikabili nchi nyingi za afrika kushindwa kusambaza maji kwenye maeneo mbalimbali.

UM waitaka Myanmar kuharakisha maendeleo ya demokrasia

Mjumbe wa Umoja wa mataifa ailiyeko ziarani nchini Myanmar amezihimiza mamlaka nchini humo kuweka nguvu zaidi kwenye ujenzi mpya wa demokrasia na maridhiano ya kitaifa hasa katika kipindi hiki ambacho taifa hilo linaanza safari mpya.

UNICEF kusambaza neti za kuzuia mbu katika mkoa wa Cunene nchini Angola

Shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF kwa ushirikiano na mpango wa kupambana na ugonjwa wa malaria nchini Angola watatoa neti za kuzuia mbu kwa watu hususan watoto kwenye mkoa wa Cunene nchini Angola

Hatua iliyopigwa Kenya kutimiza lengo la milenia la usawa wa kijinsia

Tatizo la kutokuwepo kwa usawa wa kijinsia katika nchi nyingi zinazoendelea bado ni kubwa.

IOM yaendelea na juhudi kuwasaidia wahamiaji kutoka Ethiopia waliokwama Yemen.

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM linatarajiwa kurejea shughuli ya kuwarejesha nyumbani takriban wahamiaji 2000 kutoka Ethiopia ambao wamekwama kaskazini mwa Yemen kurejea makwao.

Maonyesho ya mandeleo ya nchi za kusini mwa ulaya yakamilika Geneva

Maonyesho kimaendeleo ya juma moja ya nchi za kusini mwa Ulaya yaliyokuwa yamendaliwa mjini Geneva yamekamilika hii leo huku washirikia wakionyesha na kubadilishana zaidi ya suluhu 100 ambazo zinaweza kusaidia kutimizwa kwa maelngo ya maendeleo ya millenia.

Wanajeshi zaidi ya UM watumwa nchini Ivory Coast

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeamuru kutumwa kwa wanajeshi zaidi wa kulinda amani wa umoja huo kwenda nchini Ivory Coast kabla ya awamu ya pili ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kuandaliwa tarehe 28 mwezi huu.

Maendeleo katika huduma za simu na mtandao yaimairisha mawasilino katika nchi za Asia na Pacific

Serikali kwenye nchi za Asia na Pacific zimeafikiana kuimarisha miundo mbinu ya mawasiliano ambayo itachangia kuwepo kwa maendeleo katika huduma za mawasiliano ya simu za mkononi na kwenye mtandao kama moja ya njia za kuimarisha maendeleo.