Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon jana Jumapili amefanya mkutano maalumu na Rais Paul Kagame wa Rwanda kando na mjadala wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.
Tume huru ya kimataifa iliyoteuliwa na Rais wa baraza la haki za binadamu kuchunguza tukio la meli ya flotilla Gaza Mai 31 mwaka huu imewasilisha ripoti yake kwa baraza hilo.
Kwa upande wake makamu wa Rais wa Sudan Ali Osman Taha alizungumza kwenye mkutano maalumu kuhusu hali ya nchi yake amesema wanajidhatiti na jukumu lao.
Kando na mjadala unaondelea kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon jana usiku aliitisha mkutano maalumu wa kujadili suala la Sudan.