Habari Mpya

Zaidi wa wakimbizi 100,000 kutoka Afghanistan warejea nyumbani mwaka huu

Idadi ya wakimbizi wa Afghanistan wanaorejea makwao kutoka Pakistan na Iran imepanda na kufikisha wakimbizi 100,000 mwaka huu ikiwa ni mara mbili zaidi ya mwaka uliopita kulinganana ripoti ya umoja wa mataifa.

Kamishna wa Haki za Binadamu UM alaani vikali mauwaji ya wahamiaji 72 chini Mexico

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya Haki za Binadamu Navi Pillay ameelezea masikitiko yake kutokana na mauwaji ya wahamiaji 72 nchini Mexico yaliyofanywa katika eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo.

Watu milioni 1.3 hufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani : UNECE

Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Ulaya, UNECE pamoja na shirikisho la kimataifa la mpira wa vikapu FIBA, zimezindua Alhamisi kampeni mpya ya kupasha habari juu ya usalama barabarani wakati sambamba na kufunguliwa kwa mashindano ya Mpira wa vikapu duniani yanayoanza Uturuki kuanzia Agosti 28 hadi Septemba 12.

Mapinduzi ya kilimo Afrika yanahitaji juhudi za dhati za kila mtu UN

Mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa cha maendeleo ya mashambani, Kanayo Nwanze, amesisitiza haja ya hii leo ya kuwepo na sera kabambe, uwezo wa kufika katika masoko, miundo mbinu na teknolojia za bei nafuu ili kuhakikisha usalama wa chakula barani Afrika.

Rais wa Brazil ajiunga na kampeni ya FAO ya kupambana na njaa duniani

Rais Luiz Lula da Silva wa Brazil amejiunga na kampeni ya kimataifa ya kupambana na njaa iliyotayarishwa na idara ya Chakula na Kilimo FAO, kwa kutiasini jina lake kwenye waraka ya kimataifa ya FAO ya kupambana na njaa iliyopewa jina la "bilioni1njaa" na akapuliza firimbi manjano ya kampeni hiyo iliyopewa jina la " firimbi dhidi ya njaa".

Jumuia ya Kimataifa imelaani al-Shabab kwa mashambulizi dhidi ya raia wa Somalia

Norway, Marekani ofisi ya Umoja wa Afrika huko Somalia Umoja wa Ulaya, IGAD, Umoja wa nchi za Kiarabu, pamoja na ofisi ya masuala ya kisiasa ya Umoja wa Mataifa kwajili ya Somalia, zimetoa taarifa ya pamoja Alhamisi kulaani vikali mashambulizi yanayoendelea dhidi ya wakazi wa Mogadishu, yanayofanywa na wanaharakati wenye siasa kali wa kundi la al-Shabab.

MONUSCO inatathmini upya shughuli zake DRC kufuatia ubakaji wa watu wengi

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, MONUSCO Roger Meece amesema ofisi yake inatafakari upta juu ya shughuli zake huko mashariki ya Kongo kufuatia ubakaji wa watu wengi ulofanywa na makundi ya waasi.

UN inaimarisha huduma Pakistan wakati mafuriko yawaathiri watu 17

Umoja wa Mataifa umeimarisha juhudi zake za huduma za dharura huko Pakistan wakati idadi ya wanaoathirika na janga hilo mbaya imefikia watu milioni 17.

Serikali, mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali washirikiana kulinda maeneo yenye utajiri wa viumbe Amerika ya kusini

Amerika ya kusini pamoja na nchi za Caribbean yametajwa kama maeneo yaliyo na utajiri wa sehemu nyingi za kiasili na kibaolojia duniani huku nchi za Brazil, Colombia, Equador, Mexico, Peru na Venezuela zikitajwa kuwa na kati ya asilimia 60 na 70 ya aina ya viumbe duniani.

Miradi ya kilimo katika maeneo ya nyanda za chini yenye matope nchini Liberia yatoa mazao mengi ya kilimo

Ardhi yenye rutuba ya nyanda za chini ya kilimo inayochukua thuluthi tano ya ardhi yote nchini Liberia ni moja ya mpango unaodhaminiwa na jumuia ya ulaya na shirika la mpango wa chakula duniani wa kuliwezesha taifa hilo kujitegemea kwenye zao la mchele na moja ya njia ya kuinua maisha ya jamii zinazotegemea kilimo nchini humo .