Habari Mpya

Niger inahitaji msaada wa dharura kutokana na mafuriko: OCHA

Idara ya Kuratibu Huduma za Dharura za Umoja wa Mataifa OCHA imetoa wito kwa wafadhili na mashirika ya misaada kupeleka kwa haraka sana vifaa vya kuwapatia watu hifadhi, mablanketi na vyandarua vya kujikinga na umbu, wakati mvua nyingi zina wasababisha watu kuhama huko Niger kutokana na mafuriko makubwa.

UM unalaani kuuliwa wagombea wawili na wafanyakazi wa kampeni Afghanistan

Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Afghanistan UNAMA imelaani kuuliwa kwa wagombea wanne wa uchaguzi wa bunge katika jimbo la magharibi la Herat huko Afghanistan pamoja na mauwaji ya watu watano wanaosaidia katika kampeni za uchaguzi za mgombea mmoja mwanamke katika jimbo hilo hilo.

Wakuu wa UNICEF na WFP watatembelea maeneo ya mafuriko Pakistan

Mkurugenzi Mtendaji wa Idara ya Chakula Duniani WFP, Bi. Josette Sheeran atafanya ziara ya siku mbili huko Pakistan, kutathmini jinsi kazi za shirika lake zinavyokidhi mahitaji ya mamilioni ya watu waloathirka na mafuriko, kuhakikisha uratibu mzuri na juhudi za serikali ya Pakistan na kuhimiza kuendelea kupatikana ungaji mkono wa kimataifa katika juhudi za msaada.

Mahakama ya ICC yaueleza Umoja wa Mataifa kuhusu ziara ya rais wa Sudan nchini Kenya aliyepewa waranti wa kukamatawa na mahakama hiyo

Mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu ICC imelieleza baraza la usalama la umoja wa mataifa kuwa rais wa Sudan Omar al-Bashir anayetafutwa na mahakama hiyo kujibu mashtaka ya mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya ubinadamu alizuru Kenya ambayo ni mwanachama wa mahakama hiyo nchi inayostahii kumkamata na raia Bashir.

Wataalamu wa UM wahimiza ungaji mkono zaidi kutekelezwa mkataba juu ya kutoweka watu

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wenye jukumu la kusaidia familia kujua hatima au mahala waliyopo jamaa zao walopotea anahimiza mataifa kueleza kwamba kutoweka kwa nguvu watu ni uhalifu na wasaidiye katika utekelezaji wa mkataba unaokabiliana na tatizo hili.

Ban ahimiza NGO's kuhamasisha serikali kufikia malengo ya Afya Duniani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali kuongeza juhudi zao ili kuendelea na ahadi ya kuokoa maisha ya wanawake na watoto.

Jopo la UM la mabadiliko ya hali ya hewa lasema ripoti ya tathmini huru itasaidia kazi zake

Katibu Mkuu Ban Ki-moon amepongeza kazi za baraza huru la wasomi IAC kutathmini matokeo ya jopo la ushirikiano wa serikali juu ya mabadiliko ya hali ya hewa, IPCC.

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu kuizuru Peru

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kulinda haki za binadamu anatarajiwa kufanya ziara rasmi ya juma moja nchini Peru kwa mwaliko wa serikali.

Mkuu wa UNEP akabidhi tuzo lake la Tallberg kwa waathirika wa mafuriko Pakistan

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhifadhi mazingira Achim Steiner, ametoa kiasi cha dola za kimarekani 70,000 ambazo alizipata kupitia tuzo la Tallberg ili kusadia juhudi za uimarishwaji wa hali za kibanadamu nchini Pakistan nchi ambayo iliyokumbwa namafuriko makubwa na waathiri malioni ya watu.

Afisa wa UM alaani vikali mauwaji ya waandishi wa habari Honduras

Umoja wa Mataifa umelezea kusikishwa kwake kutokana na hali ya mambo huko Hondurus ambako kumeshuhudia waandishi wa habari 9 wakiuwawa ndani ya mwaka huu pekee.