Habari Mpya

UNICEF yaridhishwa na Serikali ya Angola namna inavyokabiliana kupunguza vifo vya kina mama na watoto

Kwa mara ya kwanza Serikali ya Angola imepiga hatua kubwa katika kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto wadogo.

UNESCO yaalani vikali mauwaji ya mwandishi wa habari Indonesia

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO amelaani vikali mauwaji ya mwandishi wa habari mmoja wa Indonesia na ameitaka mamlaka inayohusika kuwaleta katika mkono wa sheria wale wote waliohusika kwenye mauwaji hayo.

Kikosi cha UM Lebanon kimetoa msaada wa magari kwa jeshi la nchi hiyo

Kikosi cha mpito cha Umoja wa mataifa huko Lebanon, UNIFIL kimelikabidhi jeshi la Lebanon magari 39 katika juhudi za kuongeza uwezo wao wa kuimarisha usalama huko kusini mwa nchi.

Mwanamitindo kutoka Iceland aibuka mshindi wa shindano la Umoja wa Mataifa kuhusu vita dhidi ya umaskini

Mwanamitindo wa picha kutoka nchini Iceland ndiye mshindi wa tuzo la shindano la matangazo la Umoja wa Mataifa linalotoa hamasisho barani Ulaya kuhusu malengo ya millenia ya kukabiliana na umaskini kabla ya mwaka 2015.

WHO yatilia shaka namna ya wanawake wanavyoongezeka kwenye uvutaji wa sigara

Shirika la afya duniani WHO limeonya kwamba wanawake duniani kote wanakabiliwa na tishio la uvutaji wa sigara na hivyo kukaribisha maradhi yakiwemo kansa.

Ban amewateuwa watu mashuhuri kuimarisha msaada wa mataifa maskini duniani

Katibu Mkuu Ban Ki-moon ameteuwa tume ya watu mashuhuri 10 kutoa ushauri juu ya msaada unaohitajika kusaidia mataifa maskini kabisa duniani kuweza kutekeleza malengo yao ya maendeleo kabla ya mkutano muhimu wa kimataifa juu ya matafifa yenye maendeleo madogo kabisa, LDC hapo mwakani.

UM unahitaji helikopta zaidi kuwasilisha msaada kwa waathiriwa wa mafuriko Pakistan

Janga la mafuriko likiendelea huko Pakistan, idara za huduma za dhaura za Umoja wa Mataifa zinakadiria kwamba watu 800,000 wanaohitaji msaada kote nchini wanaweza kufikiwa kutumia njia za anga pekee yake.

Idara ya UM inawafunza wakufunzi juu ya kupunguza hatari za janga

Warsha ya kutoa mafunzo kwa wakufunzi juu ya namna ya kupunguza hatari za majanga imefunguliwa huko Kenya kwa matumaini kwamba wanaoshiriki watatumia masomo waloyapata kwengineko barani Afrika.

Lazima kukomesha ghasia za ngono kua silaha ya vita: UNICEF

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF, Anthony Lake, anasema shambulio la ubakaji wa zaidi ya wanawake na wasichana 150 huko mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linabidi kua onyo la kusitisha utumiaji wa ghasia za ngono kama silaha ya vita.

Baraza la Usalama linalaani vikali shambulizi dhidi ya hoteli Mogadishu

Hali ya ukosefu wa usalama na wasi wasi unaendelea kuwakumba wakazi wa Mogadishu wakati waasi wa Kislamu wakiendela na mashamblizi yao dhidi ya serikali.