Habari Mpya

Uwepo wa makundi ya wanamgambo wenye silaha kunatishia hatua za amani Lebanon

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa licha ya juhudi za kuipa nguvu serikali ya Lebanon na mipaka yake, uwepo wa makundi ya wanamgambo wenye silaha unatishia amani ya nchi hiyo na ukanda mzima.

WFP kuchukua mtazamo mpya kuwasaidia watu kaskazini mwa Uganda

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linabadili mtazamo wa jinsi linavyoendesha shughuli zake katika jimbo la Karamoja linalokabiliwa na ukame kaskazini mwa Uganda.

WHO imewataka wazazi Uchina kuwapeleka watoto kupata chanjo ya Surua na Hepatitis B

Shirika la afya duniani WHO leo limewataka wazazi nchini Uchina kuwalinda watoto wao dhidi ya vifo vya mapema na matatizo ya muda mrefu ya maini kwa kuwapa chanjo ya surua na homa ya manjano au hepatitis B.

Mwakilishi wa UM amesema hofu kubwa ya MONUC DRC ni kuwalinda raia

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Alan Dos ametembelea eneo la Mbandaka na kukutana na viongozi mbalimbali wa serikali . Akiwa huko kusema hofu ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo ni ulinzi wa raia.

Tuzo ya kinara wa dunia mwaka huu imelenga uchumi unaolinda mazingira

Tuzo ya kinara wa dunia mwaka 2010, tuzo ambayo ni ya juu kabisa ya Umoja wa Mataifa kwa viongozi bora wanaojali mazingira imetolewa na washindi wametangazwa leo mjini Seoul Korea ya Kusini.

Leo ni Siku ya Kimataifa ya kuenzi dunia lakini dunia ipo katika shinikizo: Ban

Leo ni Siku ya Kimataifa ya kuienzi na kuithamini dunia. Mwaka jana mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa uliamua kuwa tarehe 22 April itakuwa siku ya kuienzi dunia mama kwa kuonyesha umuhimu uliopo wa kutegemeana baina ya binadamu, viumbe vingine na dunia.

Kumbukumbu ya chernobyl inakumbusha changamoto za mazingira

Zimesalia siku chache tuu kabla ya kumbukumbu ya miaka 24 ya zahma ya kinu cha nyuklia cha Chernobyl Ukraine iliyokatili maisha ya watu zaidi ya laki tatu.

Volkano ya Iceland yachelewesha mpango wa makazi kwa wakimbizi wa Kipalestina

Kulipuka kwa volkani nchini Iceland wiki jana kumechelewesha mpango wa kuwapa makazi kundi la wakimbizi wa Kipalestina wanaotoka Iraq.

Mfuko wa UM kushirikiana na American Idol katika kipindi malumu

Mamilioni ya watazamaji wa kipindi maarufu cha televisheni cha mashindano ya kuimba hapa Marekani American Idol watapata fursa usiku wa leo kuchangia katika shughuli za mfuko wa Umoja wa Mataifa UNF duniani kote.

FAO inatoa msaada kwa wafugaji wa Afrika ya Magharibi

Shirika la chakula na kilimo FAO limesema linaongeza msaada wake kwa wakulima na wafugaji nchini Niger na Chad kutokana na tatizo la chakula lililosababishwa na msimu duni wa mvua.