Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu ICRC limesema mauaji, ubakaji na ghasia zilizopuuzwa wakati wa kampeni za uchaguzi wa Rais mwaka jana ziliwafanya maelfu kuzikimbia nyumba zao Colombia.
Afisa wa Umoja wa Mataifa leo ametoa wito wa kufanyika juhudi kubwa kuwasaidia Waafghanistan ambao wako katika hatari kutokana na majanga ya asili, vita na kutokuwepo kwa huduma za afya.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na ukimwi UNAIDS Miche Sidibe alialikwa na serikali ya Afrika ya Kusini kwenye uzinduzi wa kampeni mpya ya upimaji wa ukimwi iliyoanzishwa na Rais Jacob Zuma.
Mpanmgo wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kwenye jimbo la Darfur Sudan UNAMID umepokea polisi wa kike 50 kutoka Ghana mwishoni mwa wiki.
Jumapili ya tarehe 25 Aprili ni siku ya malaria duniani na siku hii inaadhimishwa zikiwa zimesalia siku 250 kutimiza changamoto iliyowekwa na Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa . Changamoto hiyo ni kwa nchi zote zenye matatizo ya malaria kuweza kufikia malengo ya kudhibiti ugonjwa huo ifikapo desemba 31 mwaka huu.