Umoja wa Mataifa umesema unaunga mkono mpango wa jumuiya ya kiuchumi ya nchi za magharibi ECOWAS na Umoja wa Afrika AU kutuma ujumbe mkali kwa vikosi vya jeshi nchini Guinea-Bissau.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na washirika wake wamesema ukosefu wa maji salama na usafi mashuleni vinaathiri uwezo wa watoto kusoma na afya zao.
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na mapambano dhidi ya ukimwi UNAIDS leo limeahidi kuimarisha ushirikiano na nchi 50 zinazozungumza Kifaransa katika kupambana na ugonjwa wa ukimwi.