Habari Mpya

Dola bilioni 8 zimeahidiwa leo kwenye mkutano wa kuisaidia Haiti

Nchi na mashirika mbalimbali wameahidi kutoa zaidi ya dola bilioni nane hii leo ili kuisaidia Haiti katika ujenzi mpya baada ya kukumbwa na tetemeko la ardhi.

Nusu ya watu wa Niger wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula

Nusu ya watu wa Niger wanakabiliwa na matatizo makubwa ya chakula kutokana na mvua za masika kutonyesha na mavuno hafifu mwaka jana.

ILO imetoa wito wa kuwepo na mfumo wa haki kwa wafanyakazi wahamiaji

Utafiti uliofanywa na shirika la kazi duniani ILO wakati huu wa mtafaruku wa kiuchimi duniani umeainisha kuwa kuna haja ya kuwa na mtazamo wa haki ili kuwapa usawa wafanyakazi wahamiaji milioni 105 kote duniani.

UM umeonya kuwa ahadi za kupungua gesi ya viwanda hazitoshi kufikia malengo ifikapo 2020

Katibu mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa cha mkataba wa mabadiliko ya hali ya hewa Yvo de Boer amesema ahadi zilizotolewa na nchi mbalimbali kupunguza gesi za viwandani hazitoshelezi kufikia malengo ifikapo mwaka 2020.

ICRC imeridhishwa na kuachiliwa kwa mateka mwingine wa Colombia

Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu ICRC, limesema limeridhika na limefurahishwa na kuachiliwa kwa Sajenti Pablo Moncayo.

Mkutano wa wahisani kuisaidia Haiti umeanza leo mjini New York

Wajumbe kutoka nchi zaidi ya 130 leo wameanza mkutano katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York kwa lengo la kukusanya fedha za kuisaidia Haiti baada ya kukubwa na tetemeko la ardhi mwezi Januari.

Haiti inahitaji dola bilioni 11ili kujijenga upya katika miaka kumi ijayo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo katika mkutano wa wahisani hapa New York amesema katika miaka kumi ijayo Haiti itahitaji dola bilioni 11 kujijenga upya baada ya tetemeko la ardhi la Januari.

ICC yatoa ruksa kufanyika uchunguzi wa ghasia za baada ya uchaguzi Kenya

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC iliyoko The Hague Uholanzi leo limetoa ruksa kwa ombi la waendesha mashitaka kuchunguza uhalifu dhidi ya binadamu unaodaiwa kufanyika Kenya katika ghasia za baada ua uchaguzi mkuu miaka miwili iliyopita.

Umoja wa Mataifa unachunguza mauaji ya raia yanayoendelea Congo RDC

Umoja wa Mataifa unaendelea na uchunguzi wake kufuatia kundi la Lords Resistance Army kufanya mauaji ya raia Kaskazini Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya congo Desemba mwaka 2009.

IOM imezindua wavuti Georgia kuwasaidia wanaotaka kuwa wahamiaji

Wakati huohuo shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linazindua wavuti nchini Georgia kuwasaidia wanaotaka kuwa wahamiaji kufanya uamuzi wa mipango yao ya kusafiri ng\'ambo kutafuta kazi.